Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwasisitiza viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa (hawapo pichani)kuzingatia Utawala Bora leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam,  katika mkutano na viongozi hao wa kujadili mambo ambayo wadau wa Sanaa wanataka Serikali iwafanyie ili kuendeleza tasnia hiyo.

Muandaaji wa Filamu nchini Adam Juma aikiiomba Serikali kuboresha Elimu ya Masuala ya  Filamu katika Vyuo kwa kuweka vifaa vya kisasa vya kujifunzia, leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa kujadili mambo ambayo wadau wa Sanaa wanataka Serikali iwafanyie ili kuendeleza tasnia hiyo , uliyoandaliwa na  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Msanii wa Muziki wa Bongo Witness maarufu kama “Kibonge mwepesi” akiiomba serikali tafuta namna bora ya kukusanya mirabaha ya kazi za wasanii ili waweze kupata gawio lenye fungu kubwa kutoka vyanzo mbalimbali ambapo kazi za muziki na sanaa mbalimbali zinatumika, leo Novemba 30, 2020, katika mkutano na viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa kujadili mambo ambayo wadau wa Sanaa wanataka Serikali iwafanyie ili kuendeleza tasnia hiyo , mkutano huo uliandaliwa  na  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Wadau wa Sanaa na Viongozi wa Vyama na Mashirikisho wakifuatilia maagizo ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) akiwataka viongozi  hao wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa kuzingatia Utawala Bora, leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam,  katika mkutano na viongozi hao wa kujadili mambo ambayo wadau wa Sekta ya Sanaa wanataka Serikali iwafanyie ili kuendeleza tasnia hiyo.Baadhi ya Viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi aliyeketi (watatu kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano na viongozi hao wa kujadili mambo ambayo wadau wa Sekta ya Sanaa wanataka Serikali iwafanyie ili kuendeleza tasnia hiyo uliyofanyika leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam, Wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza na wapili  kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Ishengoma.

***************************************

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam

01/11/2020.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi ametoa siku 30 kwa viongozi wote wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa nchini kuwasilisha mikakati ya mambo ambayo wahahitaji serikali iyaboreshe ili kuongeza  tija kwa tasnia ya Sanaa.

Dkt.Abbasi ametoa agizo hiyo leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Sanaa pamoja na Wachapishaji kilicholenga kuchambua mambo ambayo sekta ya Sanaa inahitaji Serikali iyafanye kutatua mahitaji mahususi ya kuendeleza sekta hiyo.

“Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anataka Sekta ya Sanaa iboreshwe ili wasanii  waweze kunufaika na kazi zao hivyo ningependa kupata angalau mambo matano  makubwa, ambayo mnaanini serikali ikiyafanyia kazi yatasaidia  sekta hii kusonga mbele na kuleta mabadiliko chanya, ili tujenge hoja kama inavyofanyika katika sekta nyingine,”alisema Dkt.Abbasi.

Akiendelea kuzungumza Katibu Mkuu huyo na Msemaji wa Mkuu wa Serikali alisitiza Viongozi wa Vyama  na Mashirikisho hayo kuzingatia Utawala Bora na kuacha migogoro, kwani serikali haitaweza kufanya kazi  na viongozi wenye migogoro, kwani kumekuwepo na malalamiko mengi ya ukiukwaji wa Katiba na Kanuni za uendeshaji wa mashirikisho hayo, hivyo ni lazima muwe na umoja ili muweze kufanikiwa.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza  alitoa msisitizo  kwa kamati iliyoundwa kufuatilia masoko ya kazi za sanaa, kufanya utafiti wa kina ili kubaini  namna wasanii  wanaweza kushiriki katika fursa za Kitaifa na Kimataifa.

Naye mmoja wa wadau wa Waandishi wa Vitabu Tanzania Bw.Gabriel Kitua alitoa maoni kwa COSOTA kuhusu kuangalia namna ya kulinda haki za kazi za waandishi  wa vitabu kwa kuthibiti suala la udurufu wa vitabu, pia aliomba mtoa ithibati asifanye biashara kwani anapoa andika anakuwa anashindana na  wadau wanaowathibitisha na kuleta changamoto katika mauzo.

Pamoja na hayo nae Mc William Chitanda  alitoa ombi kwa serikali  la kuwa na Jengo la shughuli za Sanaa kwa kila Wilaya kwani hiyo itasaidia kukuza na kuendeleza sekta ya Sanaa katika kila eneo nchini.

Aidha, Mtayarishaji na Filamu Bw. Adam Juma aliomba serikali kuboresha elimu ya fani za Sanaa (Filamu) katika vyuo kwa kuweka vifaa vya kisasa vya kujifunzia  vyuoni,  pia aliomba serikali kutoa mwongozo wa kuzipa viwango kazi za filamu zinazozalishwa hapa nchini na kwa filamu iliyochini ya kiwango isipitishwe.

Halikadhalika katika mkutano huo Dkt.Abbasi alisema kuwa anazitaka taasisi  zinazosimamia sekta ya sanaa kutatua changamoto za wadau hao  badala ya wadau hao kutumia mawakala na  kwenda mpaka kwa viongozi wa juu wa serikali na kusema kuwa kwa ushiriki wa wasanii wa filamu katika shughuli za serikali Bodi ya filamu ndiyo itakayo ratibu na kwa Wasanii wa Muziki BASATA ndiyo wataratibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...