Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi akituma salaam kwa wana Dar es Salaam, Tanzania na Afrika
kwa ujumla kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival kuwa limewadia na
litafanyika tarehe 26,Desemba 2020 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tamasha
hilo.

Msanii Mkongwe wa
Bongo Fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID akiwahakikishia mashabiki
zake kuwa amejipanga kutoa burudani ya viwango vya hali ya juu hivyo
wasanii wengine nao wajipange kwani hili ni tamasha kubwa sana na
watanzania wanatarajia show nzuri, leo Desemba 24, 2020 Jijini Dar es
Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya
tamasha la Serengeti Music Festival.

Msanii wa Muziki
Mrisho Mpoto akitoa shukrani kwa Serikali kwa kuandaa Tamasha la
Serengeti Music Festival huku akieleza orodha ya wasanii watakoshiriki
tamasha hilo kuwa kubwa hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa
Uhuru kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii hao,katika mkutano na
waandishi wa habari uliyofanyika Jijini Dar es Salaamleo Desemba 24,
2020 .

Msanii wa Muziki wa
Hip Pop Kala Jeremiah akitoa shukrani kwa Serikali kwa kuandaa Tamasha
la Serengeti Music Festival kwani limeleta hari mpya kwa wasanii kwa na
kuonyesha dhana ya serikali kujali Wasanii na kuthamini mchango wao,leo
Desemba 24, 2020, katika mkutano na waandishi wa habari wa kutoa
taarifa ya maandalizi ya tamasha hilo, uliyofanyika Jijini Dar es
Salaam.
*********************************************
Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
24/12/2020
24/12/2020
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi ametuma salamu kwa Wana Dar es Salaam, Watanzania wote na
Afrika kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival limewadia na litafanyika
Desemba 26, 2020 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Dkt. Abbasi ameyasema
hayo leo Desemba 24, 2020 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari
kuhusu maandalizi ya tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Serikali kwa
lengo la kuanzisha uhusiano wa karibu kwa sekta ya Sanaa na Utalii.
Akiendelea kuzungumza
katika mkutano huo na waandishi wa habari Dkt. Abbasi alisema tamasha
hilo litakua ni shukran ya mchango wa wasanii wazamani ambao wamesaidia
ukuaji wa tasnia ya Muziki nchini kutoka kuonekana kama jambo la kihuni
mpaka kuonekana kuwa chanzo cha kuchangia pato la mmoja mmoja na
taifa.
“Serikali imesikia
kilio cha Wasanii wengi kuhusu Taifa kutokuwepo kwa tuzo zinazoandaliwa
hapa nchini hivyo basi mwezi Machi, 2021 tutakuwa na Tuzo. Tutaanda tuzo
hizo na Wasanii tunaomba kwa atakayeshindwa basi akubali na asiende
kulalamika popote” alisema Dkt. Abbasi.
Pamoja na hayo Katibu
Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali alisema baada ya
Tamasha hilo, tarehe 27, Desemba 2020 kutakuwa na mwendelezo wa Tamasha
la Sanaa na Utamaduni litakalofanyika Bagamoyo katika chuo cha TaSuBa,
na huko kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.
Naye Msanii wa Hip
Pop Kala Jeremiah ameishukuru Serikali kwa kuandaa tamasha hilo, huku
akisema anaamini kuwa tamasha hilo limeanzishwa katika kipindi cha
sherehe za Krismas litaendelea kuwa tamasha kubwa hapa nchini na Afrika.
Halikadhalika kwa
upande wa Msanii Khalid Mohamed maarufu kama TID alitoa shukran kwa
Serikali nakuwahakikishia watanzania kuwa amejipanga kutoa burudani ya
uhakika hivyo mashabiki zake wasikose kufika uwanjani siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...