EQUITY Tanzania leo imezindua nembo mpya ya utambuzi unaoendana na safari ya mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings. Uzinduzi huo mpya unalenga kuiweka kampuni katika njia ya ukuaji endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea katika mazingira ya sekta ya fedha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Serena Hoteli jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti alisema kuanzia sasa, Equity Tanzania itajitambulisha kwa nembo iliyobeba kikapu kilichosheheni bidhaa na huduma mbali mbali zakifedha chini ya paa moja.

Alisema nembo mpya sasa itaonyesha “Equity” bila neno Benki kama ilivyozoeleka ili kuonyesha dhamira ya kampuni ya kuwa kituo cha kutoa huduma mbali mbali jumuishi zakifedha ndani ya paa moja, huku ikiambatana na ahadi ya usimamizi imara wa uhusiano, uwezeshaji wa wateja binafsi na biashara.

“Muonekano wetu mpya unaleta uhakika wa uwezeshaji wa watu binafsi ili kupanua fursa zao katika kuleta utajiri. Tutazindua muonekano mpya katika matawi yetu yote, njia zetu za kutolea huduma zakibenki kidijitali, mitandao yakijamii, tovuti, njia zakibenki kupitia simu za kiganjani, biashara mtandaoni na mashine za kutolea fedha. Kuanzia sasa mtaanza kuona alama za nembo yetu mpya katika matawi yetu ikiwa ni sehemu ya programu yetu ya mabadiliko,” alisema Kiboti.

Aidha aliongeza kuwa wateja kwa sasa watarajie kupata huduma bora kabisa bila kuwepo na aina yeyote ya hitilafu wakati benki ikijipanga kukuza idadi ya wateja wake.

“Tutaendela kubuni huduma bora kwa lengo la kupanua upatikanaji wa huduma jumuishi zakifedha nchini kote…Tutaimarisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya simu za kiganjani na kupeleka huduma zetu mpaka maili ya mwisho kupitia Equity Wakala. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Mawakala wetu wanaendelea kujipatia pato la ziada na kutengeneza ajira mijini na vijijini. Tunaahidi kuendelea kuwa wabunifu na wenye umuhimu wakati ambapo mahitaji ya wateja wetu yanabadilika kulingana na malengo na ndoto zao,” alisema Kiboti.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi akitoa historia ya benki hiyo nchini alisema, ilianza kufanya biashara mnamo Februari 2012 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku ikiendelea kufanya vizuri kibiashara na pia ni mjumbe wa Taasisi inayosimamia taaluma ya kibenki nchini, Tanzania Institute of Bankers.

"...Ikiwa na Makao Makuu yake Dar es Salaam, Benki ya Equity Tanzania inayo jumla ya matawi 14 huku pia huduma zake zikipatikana kwa Mawakala wapatao 3,634, jumla ya sehemu za kutolea huduma 4,410 pamoja na Mashine za Kutolea Fedha 21. Benki ya Equity Tanzania ni kampuni tanzu ya Equity Group Holdings Plc, ambayo imeorodhesha katika masoko ya hisa ya Nairobi (Kenya), Uganda na Rwanda," alisema Eng. Mbilinyi.

Alibainisha kuwa Equity Group Holdings Plc pia hutoa huduma zakibenki katika nchi za Kenya, Sudani Kusini, Rwanda, Uganda, Tanzania na DRC. Equity Group Holdings Plc pia inayo ofisi ya biashara nchini Ethiopia. Alisema tangu Equity ianze huduma nchini Tanzania 2012, imekuwa ikilenga kubadilisha maisha, kujenga heshima na kupanua fursa za kutengeneza utajiri.

"Kwa kushirikiana na washirika wetu kibiashara, wateja na wadau wetu wa kimkakati, tumeweza kupata habari nyingi nzuri kutoka kwa watu mbali mbali na biashara zikielezea ni jinsi gani walivyonufaika na huduma zetu. Safari hii ya kubadilisha maisha pia imeshuhudia biashara yetu nayo ikibadilika. Tumepanua na kubadilisha mtindo wetu wa biashara kwa kiasi kikubwa sana huku tukiendelea na utamaduni wetu wa kujibadilisha na kuwa wabunifu zaidi katika kuwahudumia wateja wetu kupitia matawi na njia zakidijitali."

Alibainisha kuwa, wateja wao hawalazimiki kutembea kutoka tawi moja kwenda nyingine au kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine kwani wataweza kupata huduma zote zakifedha wazitakazo kwa yeyote yule aliyebeba nembo ya Equity, jambo ambalo alijinasibu kufanikiwa huku kazi hiyo ikiendelea. Kwa pekee aliwashukuru kwa ushirikiano wote wanaoutoa na kuahidi kuendelea kuwa pamoja wakati wa utekelezaji wa azma yenye ujasiri mwingi katika uwepo wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti kwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi wakizindua nembo yao mpya ya Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari,leo jijini Dar.Pichani kulia ni nembo iliyokuwa ikitumika hapo awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi wakizindua nembo yao mpya ya Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari,leo jijini Dar.
Pichani kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania Robert Kiboti na Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi wakipongezana mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa nembo yao mpya ya Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari (hawapo pichani),leo jijini Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti akizungumza mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari leo jijini Dar,wakati wa uzinduzi wa nembo yao mpya inayoendana na safari ya mabadiliko.
Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi akieleza historia ya benki hiyo nchini mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari leo jijini Dar,wakati wa uzinduzi wa nembo yao mpya. Mhandisi Mbililinyi alisema benki hiyo ilianza kufanya biashara mnamo Februari 2012 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku ikiendelea kufanya vizuri kibiashara na kwamba benki hiyo ni mjumbe wa Taasisi inayosimamia taaluma ya kibenki nchini, Tanzania Institute of Bankers.
Baadhi ya Wafanyakazi wa EQUITY Tanzania pamoja na Wadau wengine wakifuatiliia kwa makini uzinduzi wa nembo mpya ya utambuzi unaoendana na safari ya mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings. Uzinduzi huo mpya umelenga kuiweka kampuni hiyo katika njia ya ukuaji endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea katika mazingira ya sekta ya fedha.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Tanzania ,Ester Kitoka akiwashukuru Wageni waalikwa balimbali wakiwemo Waandishi wa Habari waliofika kwenye tukio la uzinduzi wa nembo mpya wa 
Sehemu ya viongozi Waandaminizi wa Equity Tanzania wakifuatilia kwa makini wakati wa uzindzuzi wa nembo mpya wa kampuni hiyo 
Sehemu ya Meza kuu ikishuhudia mabadiliko ya nembo mpya ya Equity Tanzania,hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...