Baadhi ya wakazi wa Chang'ombe Jiji la Dodoma wakiwa nje ya  Bucha ya Nyama Pori wakisubiri kununua nyama muda mfupi kabla ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko kuizindua rasmi Desema 20,2020, ili wananchi wapate fursa ya kununua kitoweo hicho, ikiwa ni kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kufungua bucha za aina hiyo nchi nzima. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

MWAIKENDA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko (katikati), akiingia kuzindua bucha ya nyama pori.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko akitoa sh. 10,000 kununua kilo mbili za nyama pori 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko akikabidhiwa risiti baada ya kununua nyama pori ikiwa ni ishara ya kuizindua rasmi Bucha ya kwanza ya kuuza nyama pori eneo la Chang'ombe Dodoma , ikiwa ni kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kufungua bucha za aina hiyo nchi nzima ili wananchi wapate fursa ya kununua kitoweo hicho.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Wananchi wakiwa wamefurika kununua nyama pori baada ya bucha hiyo kuzinduliwa rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo na mmilikiwa bucha hiyo baada ya kuizindua rasmi Bucha ya kwanza ya kuuza nyama pori eneo la Chang'ombe Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko  akitoka nje baada ya kuzindua.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Jane Mihanji akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TAWA,  Deogratius Sakawa wakati wa hafla hiyo.

Watoto wakiangalia michoro ya wanyama pori huku wengine wakichungulia ndani ya bucha hiyo.
Mmoja wa wateja akiwa amebeba  kilo moja ya nyama pori aliyoinunua.


 Mariam Damas (34), mkazi wa Chang'ombe ambaye alikutwa akisubiri zamu yake kununua nyama, alisema kuwa  tangu azaliwe hajawahi kula nyama pori, hivyo  kuishukuru serikali kufungua bucha ya aina hiyo na kwamba yeye na familia yake wataifaidi nyama hiyo waliyoinunua.


Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma

WANANCHI wamegombea kununua nyama pori wakati wa uzinduzi wa bucha ya kwanza ya kuuza nyama pori eneo la Chang'ombe, jijini Dodoma Desemba 20,2020.

Tukio hilo lilitokea asubuhi kabla hata ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), kuzindua rasmi, ambapo wananchi walifurika kwenye bucha hiyo inalomilikiwa na mtu binafsi kila mmoja akitaka kununua nyama hiyo iliyokuwa inauzwa kilo moja sh. 5000.

Ilibidi wahudumu wapate wakati mgumu, hivyo kuamua  kuwaorodhesha kwa majina na kila mmoja kiasi anachotaka lakini isizidi kilo mbili ili kila mmoja apate.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali mstaafu, Hamisi Semfuko ambaye naye alinunua kilo mbili na kupatiwa risiti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa duka hilo. Wajumbe wengine wa Bodi walinunua nyama hiyo wakiwemo wanahabari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Semfuko alisema kuwa TAWA imeamua kuzindua duka hilo kuitikia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ya kufungua bucha za aina hiyo kwa nchi nzima, ili wananchi wawe wanafaidi rasilimali za nchi yao.

Alisema  bucha hiyo ni ya kwanza na wataendelea kufungua zingine katika mikoa yote ya Tanzania, pia Tawa ambayo ni msimamizi mkuu wa uwindaji wa wanyama pori nchini, itatoa leseni chache kwa watakaohitaji kuwa na mashamba ya ufugaji wa wanyama pori.

Pia, alisema kuwa TAWA itagawa mitamba kwa watakaokuwa wanaanzisha mashamba hayo, ili uzalishaji uwe mkubwa nyama ipatikane kwa wingi. Alipoulizwa ni wanyama gani watakaokuwa wanawindwa kwa ajili ya nyama, Semfuko alijibu kuwa ni wanyama wote wanaolika  nyama yao itauzwa kwenye mabucha hayo.

Alitaja nchi zingine za Afrika zizoruhusu wananchi wake kuwa na mashamba ya kufuga wanyama pori kuwa ni; Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia, hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi,hawakuficha furaha yao ambapo waliishukuru serikali  na hasa Rais John Magufuli kwa kuwakumbuka kupata kitoweo hicho adimu.

Mariam Damas (34), mkazi wa Chang'ombe ambaye alikutwa akisubiri zamu yake kununua nyama, alisema kuwa  tangu azaliwe hajawahi kula nyama pori, hivyo  kuishukuru serikali kufungua bucha ya aina hiyo na kwamba yeye na familia yake siku hiyo wataifaidi nyama hiyo.

"Tunashukuru ana serikali kutufungulia bucha hii ya wanayama pori, mi nilikuwa naikia tu kuwa kuna nyama pori, tangu nizaliwe ijawahi kula, nasikia ni tamu sana, ila leo mimi na familia yangu tutakula kwa mara ya kwanza," alisema Mariam.

Mzee Joseph Barabara mkazi wa Mjimwema, Dodoma anayekisiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 70, alikutwa akishangaa umati uliofurika na kuuliza kulikoni? alipoambiwa ni hafla ya uzinduzi wa bucha ya kuuza nyama pori, alishukuru na kunyoosha mikono yake juu, alipoambiwa bei ya kilo moja ni h. 5000, alisema uwezo wake ni mdogo anachoweza kununua ni utumbo ambao bei yake anaweza kuimudu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...