HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea yagawa pembejeo bure kwa wakulima wa zao la ufuta

Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imegawa mbegu ya ufuta bure kwa wakulima wa zao la ufuta katika Kata ambazo zinazalisha zao hilo kwa wingi kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020 /2021.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri hiyo Bw Simon Bulenganija amesema ametumia kiasi cha sh. milioni 10 kwa ajili ya kununua mbegu hiyo kwa lengo la kuwasaidia wakulima ili waweze kuongeza uzalishaji kutoka gunia tatu hadi tano kwa ekari moja,tofauti na awali wakulima walikuwa wakizalisha gunia moja hadi tatu kwa ekari moja kwakutuia mbegu ya kienyeji.

Ametaja idadi ya kilo zilizonunuliwa na kusambazwa kwa wakulima kuwa ni kilo 1000 na aina ya mbegu ni Lindi  02 zilizonunuliwa kutoka Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Naliendele  kilichopo  Mkoani Mtwara.

Amezitaja kata na idadi ya kilo zilizosambazwa kuwa ni kata Muhukuru Barabarani na Lilahi ambao wamepata kilo 225,Kata ya Matimira  kilo 180,Kilagano kilo 180,Kizuka 180,Ndongosi kilo 90  na Magagura kilo 90.

Bulenganija ameyataja malengo ya kusambambaza mbegu hiyo ni  kuwapunguzia wakulima gharama ya kununua mbegu ya ufuta ambayo huuzwa shilingi 10,000 kwa kilo moja pia kuongeza uzalishaji na Serikali iweze kupata mapato kupitia ushuru unaotolewa na wakulima mara baada ya kuuza kupitia vyama vyao vya ushirika.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Mazao wa Halmashauri hiyo Norbert Rugonza amewashauri  wakulima wa zao la ufuta wasitegemee matokeo chanya kwenye  kilimo bila kusimamia vizuri na  kufuatilia wakati wa uzalishaji.

Amesema wakulima ambao wamebahatika kupata mbegu hizo wanatakiwa kuzitumia kama shamba darasa kwakuzalisha kwa wingi na kusambaza kwa wakulima wengine kwenye msimu wa kilimo wa mwaka 2021 /2022.  

Amesema mbegu ya aina ya lindi 02 ni mbegu bora na nzuri kwa kilimo cha ufuta kwa sababu ni mbegu ambayo inastahimili magonjwa hivyo ni vema wakulima wakaachana na dhana potofu ya kwamba mbegu za kisasa zina matatizo ya kushambuliwa na magojwa na wadudu jambo ambalo halina ukweli.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wa  Halmashauri ya Wilaya ya Songea Shekiel Masawe amesema katika msimu wa mwaka 2018/2019 ilifanikiwa kuzalisha zao la ufuta kilo milioni 1,316,227 na katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 ilizalisha zao la ufuta kilo milioni 2,378,172 na kufanikiwa kuingiza mapato ya Zaidi ya shilingi milioni 400.

Imeandaliwa na

Jacquelen Clavery

Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Songea

Desemba 8,2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...