Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Ottimale Technologies, Ally Abdallah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza uzinduzi wa huduma ya Vusha app ambayo itajihuisha na masuala ya usafirishaji wa mizigo na abiria pamoja na upatikanaji wa kazi kwa madereva wengi nchini, uliyofanyika leo katika ofisi zao zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. wengine pichani ni Mkuu wa kitengo cha Teknolojia Alfred Lukatila (Kushoto) pamoja na Msanifu Mkuu Joseph Mashauri.  
 
Mkuu wa kitengo cha Teknolojia Alfred Lukatila akionyesha namna App ya Vusha inavyo fanya kazi katika uzinduzi wa huduma hiyo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliyofanyika leo katika ofisi zao zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
 
 
****************
Kampuni ya Ottimale Technologies imezindua huduma ya Vusha app ambayo itajihulisha na masuala ya usafilishaji wa mizigo na abiria pamoja na upatikanaji wa kazi kwa madereva wengi nchini.

Akizungumza hayo mapema leo hii, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ally Abdallah amesema lengo la Vusha app nikupunguza adha ya usafirishaji wa mizigo na abiria pamoja na upatikanaji wa kazi kwa madereva mbalimbali nchini.

Ameongeza kuwa huduma ya Vusha App ni huduma iliyobuniwa baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu katika maeneo mbalimbali nchini ili kutatua kero ya upatikanaji wa huduma za usafiri ulio nafuu na uhakika kwa wafanyabiashara,wakulima na wananchi wote kwa ujumla.

  "Vusha app ni huduma iliyobuniwa na kuanzishwa na kampuni yetu baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu katika maeneo mbalimbali nchini ili kutatua kero ya upatikanaji wa huduma za usafiri ulio nafuu na uhakika kwa wafanyabiashara, wakulima na wananchi wote kwa ujumla"Amesema Ally.

Pia amesema kuwa katika wakati huu wa awali, madereva wanaohitajika kusajiliwa na huduma hiyo ni wasiopungua 3,000 katika mikoa minne ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Mbeya na Mwanza.

Hivyo wito umetolewa kwa wamiliki wa magari ili kuweza kupata kipato cha ziada na cha uhakika basi wajiunge na Vusha app ili kuweza    kuanganishwa na wateja kwa urahisi na usalama. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...