Hatua hiyo inatajwa kuifunga milango kwa mpinzani wake Donald Trump, katika jitihada zake za kisheria za kuyageuza matokeo ya uchaguzi wa 2020. Hatu hiyo inafanyika huku mteule huyo akimkosoa mpinzani wake huyo kwa maneno makali tangu kumalizika kwa uchaguzi kwa kumwita mpinga matakwa ya umma na mkaidi katiba ya nchi.

Wakati Biden akipiga kampeni ya kuunganisha taifa, baada ya uchaguzi uliowagawa Wamerekani, wajumbe kutoka majimbo yote jana Jumatatu, kwa matokeo stahiki ya kura za wajumbe zinazohitajika  270. Hatua hiyo maana yake ni kumsafishia njia sasa kuekea kuingia katika ofisi za Ikulu ya Marekani Januari 20.

Hatma ya Urais wa Marekani, kwa Trump itasalia kuwa ndoto

Kimsingi Biden alifikia hatua ya uhakika wa ushindi baada ya nyongeza ya kura 55 za jimbo la California. Na pia baada ya Hawaii kumfanya  kuongeza idadi ya kufikia jumla ya kura 306. Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump alipata 232.

Utaratibu wa kura za wajumbe, ambao umedumu kwa takribani miaka 200, umepiga msumari wa mwisho kwa kusema matakwa ya umma yamezingatiwa pamoja na kutokea purukushani za hapa na pale. Na Trump kukataa kukubali kushindwa. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...