Kutoka Asia hadi Ulaya, Marekani hadi Afrika, wimbi jengine la maambukizo ya virusi vya corona linaripotiwa kuanza rasmi na tayari idadi ya watu walioambukizwa na kupoteza maisha inatajwa kupanda kwa kasi.

Kutoka Asia hadi Ulaya, Marekani hadi Afrika, wimbi jengine la maambukizo ya virusi vya corona linaripotiwa kuanza rasmi na tayari idadi ya watu walioambukizwa na kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID-19 inatajwa kupanda kwa kasi. 

Korea Kusini tangu Januari ilifanikiwa pakubwa kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona kutokana na hatua zake za kuwataka raia kuvaa barakoa na kuwazuia kusafiri lakini pia ikizuia watu kwenda kwenye mikusanyiko.

Hata hivyo, taasisi ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa ya KDCA imeripoti rekodi mpya ya maambukizi ya kila siku iliyofikia visa 1,030 juzi Jumapili na 718 jana Jumatatu.

Moon Jae In amesema kwenye hotuba hiyo kwamba huu ni wakati muhimu kabisa kwa watu wa taifa hilo kwa ujumla kujitoa kwa dhati na kwa uwezo wao wote kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo, akiongeza kuwa wako katika wakati mgumu mno.

Kuanzia leo, shule za mjini Seoul na maeneo jirani zitafungwa na wanafunzi watasoma kwa njia ya mtandao hadi mwishoni mwa mwezi huu, huku watumishi wa huduma za muhimu tu wakiruhusiwa kwenda ofisini na mikusanyiko itakakayoruhusiwa ni ya watu chini ya 10. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...