Mkuu wa Wilaya ya Butiama AnnaRose Nyamubi (kushoto) akizungumza na timu maalum ya utaoji wa Mafunzo kwa Kamati ya ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto Kitaifa ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Jinsia Grace Mwangwa (kulia) ilipofika ofisini kwake Wilayani Butiama.Mkuu wa Wilaya ya Butiama AnnaRose Nyamubi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kwa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama wakati akifungua mafunzo kwa kamati hiyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjM8gcO1TLKwuSFJwueE2kcFttvm4gCnjA7QsAN780YQMWpwtigcNP-XWxrc5ZiUanL1Df0M5jpwbdPlImitudDOwmoaR9eEUE2ZY6Yb7vooss3RGP9OkiTz1-H-mHzFxxsmwYd-g/w640-h426/3.jpg)
Na Mwandishi Wetu Butiama Mara
Inaelezwa
kuwa jumla ya Kamati za Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto 16343 zimeanzishwa
katika mikoa Halmashauri, Kata na Vijiji ili kuongeza nguvu katika
mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na
Watoto.
Hayo yanesemwa Wilayani Butiama mkoani Mara na Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii Grace Mwanga wakati wa mafunzo kwa kamati ya
ulinzi ya Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri hiyo.
Grace amesema
kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
imeweza kuratibu mafunzo kwa Kamati hizo kwa kushirikiana na Shirika la
UNFPA ili kuzipa nguvu Kamati hizo katika kutekeleza majukumu yake.
Ameongeza
kuwa Wizara inatekeleza Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi
ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unaolenga kupambana na kutokomeza
vitendo vya ukatili kwa asilimia hamsini nchini.
Akifungua
Mafunzo kwa Kamati ya ulinzi wa Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri ya
Wilaya ya Butiama, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. AnnaRose Nyamubi amekema
vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji na mimba za utotoni
vinavyokatisha ndoto za watoto hasa wa kike za kuendelezwa katika kupata
elimu.
Ameongeza kuwa Wilaya ya Butiama imejipanga katika
kuhakikisha inapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo
yao kwa kushirikiana na wajamii husika wakiwemo wazee wa mila, watu
mashuhuri na viongozi wa dini ili kuhakikisha vitendo vya uaktili dhidi
ya wanawake na watoto vinatokomea.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Butiama Mhe. Jumanne Sagini anasema nguvu ya viongozi wa kisiasa
inahitajika katika kuhakiksha wanahusika katika mapambano dhidi ya
vitendo vya ukatili.
“Sisi viongozi wa siasa tuwajibike kwa
nafasi zetu tuoaze sauti kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya wananwake
na watoto kwani inawezekana tukiamua kwa pamoja” alisema
Naye
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Butiama Joseph Mgabu amesema kuwa viongozi
wa kidini wana jukumu kubwa sana katika mapambano dhidi ya vitendo vya
kikatili hasa katika kutoa elimu kwa waumini wao katika nyumba za ibada
amnayo itasaidia jamii kujua madhara ya vitendo hivi.
Kwa upande
wake Bi. Hesha Kisibo ameiomba jamii kuachana na mfumo dume
unaowakandamiza na kuwanyimwa wasichana na wanawake haki zao hivyo
kusababisha kutokea kwa vitendo vya kikatili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...