Na.Mwandishi wetu Arusha.

Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa  Elisante Ole Gabriel amezindua  maabara mbili  ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA),Tengeru katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Akizungumza katika hafla fupi ya Uzunduzi wa maabara hizo Profesa Ole Gabriel alisema kuwa sekta ya Mifugo inathamani kubwa katika kuhakikisha kuwa inachangia Pato la Taifa kwa kiwango kikubwa,lakini bado haijafanya hivyo.

Ole Gabriel alisema kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa kuwa itawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo hali ambayo itaongeza uwezo  katika masomo yao.

Aidha alisema kuwa Sayansi inahitajika katika kuhakikisha kuwa wafugaji wanabadili ufugaji na kuwa na Mifugo Bora zaidi pamoja na mazao yenye thamani ambayo yanatokana na Mifugo.

"Tunahitaji Sana Sayansi ya Mifugo ambayo itatusaidia kupata nyama bora,maziwa bora na hata bidhaa nyingine zote ili basi idadi tuliyonayo ya Mifugo iendane na thamani ya Mifugo yetu na hivyo tutapata Mifugo Bora zaidi"alisema Profesa Ole Gabriel

Hata hivyo alisema kuwa uwepo wa maabara hizo mbili pamoja na vifaa vitawezesha wanafunzi hao ambao wanakwenda kusaidia wafugaji wa chini katika kuhamilisha na kuchanja Mifugo kubobea katika sekta hiyo na Mifugo kuwa Bora zaidi.

Pia alisema kuwa mpango wa wizara hiyo bado ni kuboresha  kosafu na mbari za mifugo,ili kupata Mifugo bora na bidhaa bora zaidi na hatimaye kuchangia Uchumi kwa asilimia 15 tofauti na Sasa Ambapo sekta hiyo inachangia 7.64.

Nae Mtendaji  Mkuu  wa Wakala wa  Vyuo vya Mifugo wa dkt.Pius Mwambene alisema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuboresha mafunzo  na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanawasaidia wafugaji katika kubadili  ufugaji wa mazoea.

Alisema  kuwa  ni  azma  ya Serikali kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu Mbali Mbali ili kuhakikisha kuwa sekta ya mifugo inachangia ipasavyo  pato la taifa.

Nchi ya Poland imekuwa ikiisaidia Serikali katika sekta ya Mifugo katika kuhakikisha kuwa inaongeza thamani ya mifugo ili kuongeza tija katika sekta hiyo.

Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel wa Tatu Kushoto akiwa pichani na Viongozi Mbali Mbali Mara baada ya Uzinduzi wa Maabara hizo.

Katubu mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla hiyo fupi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...