Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

SIRI imefichuka kuhusu kiasi cha fedha Sh.Milioni 700 ndicho ambacho kimetumika kumbakisha mchezaji wake mahiri na mwenye ubora wa hali ya juu Cleotas Chota Chama 'Triple C'

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Desemba 2,2020 jijini Dr es Salaam Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Muhina Kaduguda ameweka mambo hadharani kwamba Muwekezaji Mohamed ana mapenzi makubwa na Simba kiasi cha kutoa Sh.Milioni 700 kumbakisha Chama ilimradi tu timu iendelee kufanya vema.

"Mo Dewji anafanya kazi nzuri na kubwa,amekuwa akitoa fedha zake kwa kujitolea si jambo ndogo na hivi karibuni  kambakisha mchezaji Cleotas Chama hapa na hakuna kelele tena au nyie hamjui? Je mnasikia tena kelele na kufanya upande wa pili kunyamaza  si kazi ndogo,"amesema.

Kaduguda amesema kutoa fedha hizo kumbakisha mchezaji huyo sio jambo, na kwa wale watu wazima wanafahamu kutoa fedha kumpa mtu ambaye sio ndugu yako wala huna udugu naye,unathibitisha mapenzi Mo kwa Simba.

Kuhusu mechi ya marudiano dhidi ya timu ya nchini Nigeria ya  ya timu FC Plantineua
 itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, amesema hawataibeza timu wanayocheza nayo kwani ni bora na inacheza mpira wa kiwango cha hali ya juu.

Katika mchezo wa awali Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plantinueua lakini haina maana watawabeza, bali wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

 Amefafanua  Fc plantineua si timu ya kubeza kwani ni miongoni mwa timu kubwa nchini Nigeria na kwamba kuwangusha vigogo kama Enyimba si jambo jepesi, hivyo amewataka mashabiki wa  Simba kuomba dua ili kupata ushindi katika mechi ya marudiano.

Hata hivyo amesema wanafahamu wanaotakiwa kuingia uwanjani katika mchezo huo ni watu 30,000 ,hivyo amewataka mashabiki ,wapenzi na wakereketwa kwenda uwanjani na safari hii hawataki kuona rangi nyingine tofauti na Simba katika mchezo huo.

Awali Kaduguda ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wachezaji wa Simba pamoja na benchi lote la ufundi kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kuibuka na ushindi tena nchini Nigeria na kufanya Simba kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki na Katie kuibuka na ushindi nchini humo.

Amewapongeza pia mashabiki,wanachama na wakereketwa wa Simb kutokana na ushindi huo na kwamba kila.mmoja ana mchango wake kwenye ushindi uliopatikana,hivyo waendelee kuiombea timu hiyo ifanye vizuri zaidi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...