
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe.
Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na bodaboda wa
Manispaa ya Bukoba mara baada ya kukutana na ushirika wao ili kuona
changamoto ambazo wanakabiliana nazo na kuhaidi kuzifanyia kazi
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe.
Neema Lugangira (Mb.) leo amekutana na Chama cha Ushirika wa Bodaboda
Manispaa ya Bukoba kuwashukuru na kuwapongeza kwa namna ambavyo
walishiriki katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020.
Katika
utambulisho, Mwenyekiti wa Bodaboda Manispaa ya Bukoba Abdul
Salum Mashankara alisema Chama hicho cha Ushirika wa Bodaboda Bukoba
Manispaa kilianzishwa Septemba 30 mwaka huu chini ya usimamizi wa Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, Mhe Brigedia Jenerali Marko Gaguti wakiwa jumla ya
wanachama 130.
Mwenyekiti huyo aliwasilisha ombi kwa kumuomba Mbunge
Neema kuungana na Mkuu wa Mkoa katika jitihada zake za kuwaunga
mkono na kuwapa ushirikiano wa kimaendeleo bodaboda.
Mwenyekiti
alisema lengo la kuanzisha ushirika huo ni kutengeneza uchumi endelevu
wa waendesha bodaboda wanakihusisha kupatiwa huduma ya mikopo na
shughuli nyengine ikiwemo kubadilisha maisha ya wanachama wao.
Aidha
alisema pia lengo ni kuwa na miradi itayotengeza ajira ikiwemo viwanda
na hatimae ushirikia huu utaweza kuwasaidia kutoka kwenye utegemezi kwa
leo mfano leo bodaboda waliowengi wanatumika kutokana na kwamba wana
mikataba na inayowafanya kushindwa kutoka kimaisha kutokana na kutakiwa
kurejedha marejesho yenye riba ya hali ya juu lakini wanakubali tu maana
hawana jinsi.
“Mfano
bodaboda ni sh.milion 2.6 sisi tunarejesha milioni 4.6 ndani ya miezi
wastani 15 jambo ambalo limekuwa likituumiza sana “Alisema.
Kwa
upande wake, Mhe Neema Lugangira (Mb.) aliwahakikishia kuwa kuja kwake
ni katika jitihada zake za kumuunga mkono Mhe Mkuu wa Mkoa wa Kagera na
kuwapongeza sana kwa ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzo na
aliahidi kuendelea kushirikiana nao.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ya mikataba; Mbunge Neema alisema anafikiria ni jambo
ambalo atapanga siku ya kukutana na Mwenyekiti wa Bodaboda ili kuweza
kupata uelewa mzuri na kuipitia mikataba waliyosaini na pengine inaweza
kuwa na hoja ya kumfanya yeye aiwasilishe Bungeni kuona namna gani
mnaweza kulindwa.
Mbunge
Neema alisema baada ya kupata uelewa wa suala la mikataba atalifanyia
kazi kwa lengo la kutafta namna ya kuwapunguzia mzigo wale ambao
waliwakopeshwa pikipiki ambazo wanazitumia kwa ajili ya kujiingizia
kipato kwa njia za halali na ni imani yake kubwa suluhu itakayopatikana
itakuwa na msaada mkubwa kwa vijana wanaondesha bodaboda nchi nzima.
Kama
ilivyoada, Mhe Neema Lugangira (Mb.) aliongezea kuwa waendesha bodaboda
ni wadau wake muhimu kwenye ajenda ya lishe bora kwa sababu wamekuwa
wakiwabeba wakina mama wanapokuwa wakiwapeleka kliniki au hospitalini
kupatiwa matibabu.
Alisema
amedhamiria kuwajengea uwezo wa masuala la lishe bora ili pale watakapo
mpakia mama na mwanae wakiwa barabarani watoa elimu ya lishe bora ili
mama aelewe umuhimu wa lishe na baba aelewe umuhimu wa mama na mtoto
kupata lishe bora na alisema anaamini hatua hiyo itasaidia kuhamasisha
lishe bora kufanyika kwa vitendo ngazi ya kaya.
“Kwani
wao kama wanaume wanaweza kuwa mabalozi wazuri kwa kushawishi wanaume
wenzao ikiwemo na wao wenyewe kubeba agenda ya lishe na kuhakikisha mama
mjamzito, mama mjamzito na mtoto chini ya umri wa miaka mitano anapata
lishe bora maana maana mara nyingi mzigo wa lishe mnatuachia sisi
wanawake nyie mnakula huko mkiwa katika mihangaiko huku wakina mama
mnatuachia bajeti ndogo tunakuwa hatupati lishe ya kutosha” Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...