Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato ( Mb.) akizungumza na viongozi wa Idara na Taasisi tajwa hapo juu.( hawamo picha) Viongozi mbalimbali wa Idara ya Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, viongozi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji ( EWURA), wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati  Eng. Marwa Petro ( hayumo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo kwenye ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo Mtumba jijini Dodoma.  

Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati Eng. Marwa Petro, ( kushoto kwa Naibu Waziri Byabato) akiwasilisha mada wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato ( Mb.) na viongozi wa Idara ya Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati pamoja na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) katika kikao cha kiutendaji kuhusiana na Sekta ya Petroli na Gesi kilichofanyika leo kwenye ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba , jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...