Askofu msaidizi wa Kanisa Katoliki Arusha mhashamu Prosper Lyimo
(kulia) akiongoza misa ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Mirerani, wapili kulia ni mgeni rasmi wa harambee
hiyo mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka na Paroko wa
Parokia hiyo Vincent Ole Tendeu, kulia ni mfanyabiashara maarufu wa
madini ya Tanzanite, Siria Meibuko ambapo zilizopatikana shilingi
milioni 50 zilipatikana.
Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, mhashamu Prosper Lyimo
(kulia) akiweka wakfu Kanisa jipya la Parokia ya Mirerani, ambapo
mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka (kushoto)
aliongoza harambee na kupatikana shilingi milioni 50.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka
(mwenye suti nyeusi) akiingia kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Mirerani, ambapo shilingi milioni 50 zilipatikana.


MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole SENDEKA
amesema kauli ya Waziri wa Madini Dotto Biteko imelenga kudhibiti
utoroshaji wa madini na siyo kuzuia wachimbaji wadogo wa madini kuwa
na Tanzanite.

Hivi katibuni, Waziri Biteko alitoa agizo la kufuta leseni kwa
wamiliki wa migodi ya Tanzanite na madalali watakaobainika kushiriki
utoroshaji wa madini ya Tanzanite na udanganyifu.

Hata hivyo, wachimbaji hao wadogo wanatakiwa kuuza madini hayo ndani
ya ukuta au kupita nayo lango la ukuta baada ya kulipa kodi kuliko
kuyapitisha kwa wizi na kuingia hatiani.

Ole Sendeka aliyasema hayo wakati akiongoza harambee ya ujenzi wa
kanisa katoliki, jipya la Mji mdogo wa Mirerani, ambapo zilipatikana
shilingi milioni 50 ikiwemo fedha taslimu na ahadi.

Alisema kauli ya Waziri Biteko imetafsiriwa tofauti kwani wanaApolo
ndiyo nguvu kazi ya uchimbaji na hawalipwi mishahara hivyo wanapaswa
kupata mgao kupitia madini.

Alisema baadhi ya wadau wa madini hawakuelewa agizo la Waziri Biteko
ndiyo sababu imesababisha sintofahamu juu ya maslahi ya wanaApolo.

"Lengo ni kuhakikisha kutowepo na wizi wa madini au udanganyifu ila
maslahi ya wanaApolo lazima yaangaliwe kwani wao ndiyo nguvu kazi na
bila hivyo shughuli hazitafanyika," alisema Ole Sendeka.

Alisema ni vyema wamiliki wa migodi wakae kwa pamoja na kuzungumza na
wanaApolo ili wafahamu hatima yao juu ya maslahi ili kuondokana na
sintofahamu iliyopo hivi sasa.

Askofu msaidizi wa jimbo kuu Katoliki Arusha, mhashamu Prosper Lyimo,
akizungumza kwenye harambee hiyo aliwashukuru wote waliojitolea
kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.

Askofu Lyimo alisema pindi watu wakutanapo hata chini ya mti kwa lengo
la kusali, kumuomba na kumshukuru Mungu hilo ni kanisa, hivyo
anawapongeza waamini kwa kujitolea ujenzi huo.

"Nawashukuru wote kuanzia mgeni rasmi Ole Sendeka, waamini wote,
jumuiya zote, vyama vya kitume na wadau wote wa maendeleo waliojitolea
kwa ajili ya ujenzi wa kanisa," alisema.

Awali, katibu wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo Raphael Ombade
alisema gharama zitakazotumika kwenye ujenzi huo ni shilingi milioni
900.

Ombade alisema ujenzi wa kanisa hilo utajengwa kwa awamu nne ikiwemo
msingi, ukuta, upauzi na kisha umaliziaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...