Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameonyesha kutoridhishwa na zoezi la majaribio ya uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi kwenye machinjio ya kisasa Vingunguti baada ya kubaini kasoro za uendeshaji wa mtambo hiyo.

Miongoni mwa kasoro alizobaini RC Kunenge ni pamoja kukosekana kwa utaalamu wa uendeshaji wa mitambo, Zoezi la uchinjaji kutumia muda mrefu kuanzia hatua ya Kwanza Hadi mwisho, kukwamakwama kwa vifaa kwa baadhi ya maeneo, Kazi nyingi kufanywa na binadamu badala ya mashine Na  wafanyakazi kufanya kazi kwa kubahatisha jambo lililopelekea Ng'ombe mmoja kutumia zaidi ya nusu saa Hadi kukamilika badala ya dakika 10.

Kutokana na hayo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi wa ufungaji wa mashine, Mshauri wa Mradi, NHC na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kufika ofisini kwake Alhamis ya Disemba 3 saa nne asubuhi.

Aidha RC Kunenge amewaelekeza NHC kuongeza kasi ili Ujenzi wa jengo ukamilike kwa wakati huku akimuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwa mkali.

Pamoja na hayo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi wa ufungaji wa mitambo kuhakikisha anatoa elimu ya matumizi ya mitambo kwa wafanyakazi ili waweze kuzitumia.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...