Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi kutembelwa maonesho ya Circus Africa yanayoendelea
katika Viwanja vya Jeshi Masaki.
Kunenge amefungua rasmi maonesho hayo ya Circus mama Africa na kutoa wito kwa wananchi kutembelea vivutio vya utalii.
Akizungumza
baada ya kuzindua, Kunenge ameipongeza bodi ya utalii Tanzania (TTB)
kwa kuendelea kuwa wabunifu Katika kuendeleza sekta ya utalii ikiwa ni
pamoja na kuweka gharama nafuu ili kuwezesha kila mwananchi kumudu.
Tamasha hilo la Circus mama Africa linahusisha utalii wa michezo ya jukwaani na vivutio vya utalii.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa
maonesho hayo yatadumu hadi Januari 10 2021, na yatahusisha michezo
mbalimbali.
Amesema,
watanzania wajitokeze kwa kwani hii ni michezo yao na inachezwa na
watanzania wenyewe kwahiyo waende wenyewe kujionea vipaji halisi.






Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge (katikati) akifurahi pamoja
na Mkurugenzi Mwendeshaji Devotha Mdachi wakati wa uzinduzi wa aonesho
ya Circus Mama Africa yanayoendelea katika Viwanja vya Jeshi Masaki.
Kikundi cha maonesho wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge akizungumza na wageni
waalikwa waliofika katika uzinduzi wa maonesho ya Circus Mama Africa
yaliyofanyika jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...