

…………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani
,mhandisi Evarist Ndikilo ,amekemea baadhi ya wawekezaji waache uhasama
na kuwekeana chuki za kibiashara na badala yake washirikiane na
kupendana ili kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda mkoani hapo.
Akizungumza na
wafanyakazi na viongozi wa uwekezaji wa SAIBABA na kampuni ya Kichina ya
Wen Xing kuhusiana na mgogoro baina ya wawekezaji hao ,Kibaha Mjini
,alimtaka mwekezaji SAIBABA kuacha vikwazo vitakavyo msababisha
mwekezaji mwenzie ashindwe kuendeleza adhma ya serikali ya ujenzi wa
viwanda.
Alisema ,tatizo kubwa
alilofikishiwa ni mpaka,hoja ya madai ya SAIBABA kutaka malipo ya dola
25,000 sawa na sh.milioni 60 kwa kampuni ya Wen Xing .
“Sasa mkoa wa Pwani
una jumla ya viwanda 1,200 na Wen Xing ni moja ya mwekezaji anaeongeza
kiwanda ,sasa SAIBABA mkianza kelele zisizo za msingi ,wakati wenzenu
wamechukua eneo ndani ya miezi saba na kujenga nyie mna miaka sita
hamjajenga toka mchukue eneo 2015 mnanishangaza !!
” Acheni visa ,ugomvi wa kibiashara, mimi kama mkuu wa mkoa siwezi kukubali visa hivi ,alisema Ndikilo.
Ndikilo alielezea
,SAIBABA kwanza walikuja na hoja ya kampuni jirani hiyo kushindwa
kununua eneo lao ,hoja ya pili kutiririsha maji na sasa hoja mpya kutaka
malipo ya dola 25,000 kinyume na taratibu hatua iliyofikia kushtaki
halmashauri hadi TAKUKURU .
Awali meneja wa Wen
Xing, Yoyo alibainisha ujenzi ulianza July mwaka huu, umefikia asilimia
60 huku,madhumuni ya kiwanda ni kutengeneza viatu,na bidhaa za plastik
,”:;,ambapo ajira ya kwanza watu 100 na wanatarajia kufikiwa 500 baadae.
Nae meneja mradi
SAIBABA ,Kanyilal Laxman alisema ,walinunua eneo mwaka 2015 na
wanatarajia kuomba kibali cha kujenga Januari 2021.
Ofisa tarafa Kibaha
Mjini,Anatoly Mhango aliwataka, wawekezaji wenye maeneo ambayo pori na
mengine kutokujengwa kwa kipindi kirefu wavijenge kabla serikali
haijachukua hatua ya kuvipokonya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...