Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) pamoja na Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) wamezungumzia umuhimu wa kilimo cha mbogamboga na matunda nchini na kwamba umefika wakatikwa Watanzania kuchangia fursa zilizopo katika kilimo hicho.

TIC na SAGCOT wamesema hayo leo wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam uliokuwa unazungumzia kongamano kubwa ambalo limeandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani(TAHA) litakalofanyika Desemba 5,2020 na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Godffrey Kirenga amesema wanapongeza TAHA na wadau wengine kwa kuandaa kongamano hilo muhimu ambalo litajadili mustakabali kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda."Ni muhimu kueleza kuna safari tumepitia katika miongo miwili iliyopita wakati sekta hii ikiwa haijulikani.

"Ilikuwa pembeni kidogo lakini nafurahi katika juhudi ambazo zimefanywa na TAHA na wadau wengine hii sekta imeeanza kuonekana moja ya sekta muhimu na kongozi katika sekta ya kilimo.Jambo muhimu katika huu mkutano.

"Kwanza kabisa kutekeleza maagizo ya Serikali, nakumbuka wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 , ilitolewa hotuba na Rais na jambo ambalo lilinifurahisha mimi na wadau wengine wa kilimo ni mikakati iliyopo kwenye kilimo,"amesema.

Ameongeza maeneo yanayokuwa kwa kasi katika kilimo ni pamoja na sekta ya mbogamboga na matunda ingawa wengi hawafahamu kwani inakuwa kwa asilia 15 kwa mwaka ukuaji, hivyo ukiweka mchango wake katika kilimo ni mkubwa.

"Sekta hii ya mbogamboga na matunda ni muhimu , na tunapata eneo jingine la kuufahamisha umma wa watanzania kwamba Tanzania iko katika ramani katika kuzalisha mboga na matunda kwa ajili ya kuuza soko la ndani na nchi jirani. "Sisi tunafanya kazi sana ukanda wa Kusini lakini haina maana kwamba tumesahau maeneo mengine, hivyo kuna umuhimu wa kuchagua ni wapi tutawekeza juhudi hizi,"amesema.

Aidha amesema kilimo cha mbogamboga na matunda kinahitaji ufahamu wa namna ya kuzalisha hayo mazao, kinahitaji miudombinu na kujipanga,hivyo lazima uwe na mbegu bora, pembejeo , kuhifadhi mazao pamoja na umuhimu wa kuwa na sera zinazotabarika ambazo zinatoa fursa za mtu kuwekeza.
"Ukiwa na sera zinazotabirika itasaidia wananchi wa Tanzania kuwekeza katika kilimo hiki, na katika eneo ambalo linatoa ajira kwa haraka ni eneo hili la kilimo cha mbogamboga na matunda.Kupitia mkutano huu naamini tutatoka na majibu ya nini cha kufanya katika kuendeleza kilimo hiki.

Hata hivyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kuendelea kutumia vyombo vyenu kuendelea kutupasha habari kuhusu fursa ambazo zinapatikana katika kilimo hiki,mkutano huu unakuja kufunguliwa na Wziri Mkuu kwetu hii ni heshima kubwa,"amesema Kirenga.

 kilimo cha nchi zilizoendelea kimejikita kwenye kilimo cha mbogamboga, ukiondoa mazao yale ya zaman, serikali inatoa kipaumbele hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasisha uwekezaji kwenye eneo hilo.

Kwa upande Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka TIC John Mnali amesema wao na TAHA ni wadau wakubwa na wanafanya kazi kwa ukaribu, hasa maeneo yale ambayo yamelengwa katika kuhamasisha na kuvutia uwekezaji nchini ikiwemo sekta ya matunda na mbogamboga.

"Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa tunafanya kazi kwa karibu sana, na kwa upande mwingine niseme tu TAHA wamekuwa wa msaada kwa kituo cha uwekezaji kwani kupitia shughuli zao wanazofanya wamekuwa mabalozi wetu wa kutangaza fursa za uwekezaji mbalimbali.

"Kupitia mkutano huu wale wawekezaji watakaonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAHA, kituo cha uwekezaji tutakuwa na jukumu la kuhakikisha wanapata vibali na leseni wanazohitaji kwa wakati, kama mavyofahamu kituo cha uwekezaji kimehamishiwa ofisi ya Rais.

"Na majukumu yetu yameongezeka zaidi, ufahamu wetu umeongezeka zaidi, tumejipanga kuhakikisha vile vikwazo kwa wawekezaji vilivyokuwepo hapo zamani vinatafutiwa suluhu.Hivyo wawekezaji wasiwe na wasiwasi kuanzisha miradi yao,TIC tumejipanga,"amesema
.

Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Godffrey Kirenga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo jijini Dar,akiipongeza TAHA  kwa kuandaa kongamano hilo muhimu ambalo litajadili mustakabali kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda,kushoto ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka TIC John Mnali

Mtendaji Mkuu wa  Asasi ya Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacqueline Mkindi akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu maandalizi ya ufunguzi wa Kongamano kubwa la Kikanda lenye lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji na kuibua fursa mpya za biashara ya mazao ya bustani nchini ambayo matunda,mbogamboga,maua na viungo.Kongamano hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,litafanyika Jumamosi,Desemba 5,2020 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...