Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2020 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila  alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo akizungumzia mafanikio waliyoyapata pamoja na namna walivyojipanga kusimamia utendaji wa wahasibu na wadhibiti wa hesabu mara baada ya changamoto ya Virusi vya Corona (COVID-19) vilivyoikumba Dunia wakati wa mkutano mkuu wa mwaka 2020 ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na kufanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitolea ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi zake pamoja na kujipanga upya kwenye utendaji wa Bodi mara baada ya kutokea kwa changamoto ya Virusi vya Corona (COVID-19) wakati wa mkutano mkuu wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wa mwaka 2020 uliofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya  wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2020 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila  akipokea zawadi kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya zamani ya NBAA, CPA  Simon Sayore(kushoto) wakati wa ufunguzi wa wa mkutano mkuu wa mwaka 2020 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2020 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...