Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocenti Bashungwa, Naibu waziri Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Dkt.Hassan Abbasi na Mratibu wa Shindano la Urembo Tanzani Bi. Basilisa Mwanukuzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa taji la Urembo Tanzania (MISS Tanzania)  Bi. Rose Manfere kwa mwaka 2020, ambaye amefika ofisi ndogo ya Mhe. Waziri Jijini Dar es Salaam Salaam Desemba 19, 2020 kwa mara ya kwanza tangu ashinde taji hilo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocenti Bashungwa akizungumza na Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2020, Bi Rose Manfere (kulia) ambaye amefika ofisi ndogo ya Mhe. Waziri Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2020   kwa mara ya kwanza tangu ashinde taji hil

 

*************************************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashugwa amempongeza Mshindi wa Urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2020, Bi. Rose Manfere kwa kutwaa taji hilo ambapo amemtaka kutumia urembo wake kuitangaza nchi vizuri.

Mhe. Bashungwa ametoa pongezi hizo leo Desemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam alipokutana na Mrembo huyo ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kumpa ushirikiano katika kutekeleza wajibu wake kwa Taifa kwa kuwa kwa sasa amebeba dhamana ya kutangaza nchi kwenye tasnia hiyo.

“Serikali tutakuunga mkono katika jukumu hili ulilopata la kupeperusha Bendera ya nchi katika tasnia ya urembo kwa mwaka mmoja, nasisitiza tumia firsa hii kutangaza utamaduni wetu, mila na desturi za taifa letu na zaidi utalii unaopatikana hapa nchini”alisema Mhe.Bashungwa.

Aidha Mhe.Bashungwa amempongeza Mratibu wa Mashindano hayo Bi.Basilisa Mwanukuzi kwa kuendesha mashindano hayo kwa weledi ambayo yamefanikisha kupatikana kwa mwakilishi wa kutangaza nchi na katika mashindano ya Urembo ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2021.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo Bi. Basilisa Mwanukuzi ameishukuru Serikali kwa kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha mashindano hayo ambapo ameahidi kuwa Mrembo huyo atafanya vizuri katika mashindano ya Dunia.

“Watanzania naomba tutoe ushirikiano kwa Mrembo huyu katika kazi yake ya kuitangaza nchi yetu kupindia urembo, akifanikiwa nchi pia imefanikiwa hivyo tumuunge mkono” alisema Bi Basilisa.

Mashindano hayo yamefanyika yamefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Slaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...