Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

ANAFAHAMIKA zaidi kama Mr Gypsum, Shaban Bruno (32) mzaliwa wa jijini Mbeya ambaye amekuwa maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii hasa Facebook na Instagram kutokana na ubunifu wa kipekee na urembo wa nyumba (interior designer.)

Akizungumza na Michuzi Blog, Shaban amesema amekuwa mtaalamu wa kazi hiyo aliyoianza rasmi mwaka 2011 na baadaye kuanzisha kampuni yake inayofahamika kwa jina la 'Gypsum Gang.'

Amesema katika kuhakikisha anafanya kazi bora aliwainua vijana wengine wapatao kumi na saba na wanafanya kazi katika Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Aidha amesema kuwa kujiajiri kumemsaidia katika kuinua kipato chake binafsi pamoja na vijana anaoshirikiana nao katika kufanya nao hizo.

Shaban amewashauri vijana kutumia fursa zinazojitokeza na kujiajiri wenyewe pamoja na kuwashika mkono vijana wengine pindi wanapofanikiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...