NA MWANDISHI WETU, BAHI
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema tafiti za kilimo cha ngano katika mikoa ya Dodoma, Mbeya na Arusha zilizofanyika hivi karibuni zimetoa matokeo chanya ambapo aina tatu za mbegu za ngano zilizofanyiwa majaribio zimeonyesha uwezo mkubwa wa kustawi nakutoa mavuno ya kuridhisha katika mikoa hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi wilayani Bahi , Naibu Waziri Bashe amezitaka taasisi za Utafiti wa kilimo (TARI), Taasisi ya Mbegu (ASA), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao nchini (DCD) kushirikiana katika kutekeleza mpango wakilimo hicho ili kupata matokeo chanya.
“Hatua hiyo inakwenda sambamba na sera ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 20 – 25 inayoelekeza taifa kuzalisha zao la ngano kwawingi ili kusitisha uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchini.” Alisisistiza
Naibu Waziri Bashe alimaliza kwa kusema kuwa, kwa kuanzia zoezi hilo litatekelezwa katika Skimu kumi na nne Wilayani Bahi.
Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo, akiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi akipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo yake aliyoyatoa Mwezi June 2020 .
Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma,Raphael Laiza akipokea Maagizo
ya Mh. Waziri Bashe, hayupo katika picha, kwenye ukumbi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Bahi.
Kulia, Mkulima wa Bahi Sokoni Sechelela Mbigili akizungumza kuhusu
athari za mafuriko katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Bahi
sokoni, kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
Mhe.Naibu
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiangalia sampuli ya ngano iliyofanyiwa
majaribio kwenye skimu ya kilimo cha Umwagiaji Bahi Sokoni.
NaibuWaziriwaKilimo
Hussein Bashe akikagua sehemu ya Madaraja yaliyojengwa na Kampuni ya
SGR ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...