Na Mwandishi wetu,Michuzi TV

NI pigo kubwa katila tasnia ya sanaa nchini! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kuripotiwa taarifa za kifo cha Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania( BASATA)Godfrey Mngereza aliyefariki dunia Desemba 24,2020.

Mngereza amefariki akiwa Hospitali ya General jijini Dodoma alipokuwa amelezwa ambapo Mwenyekiti wa BASATA amethibitisha kufariki kwa Katibu Mtendaji huyo.

Wadau mbalimbali na hasa waliokuwa katika tasnia ya sanaa nchini wameonesha kusikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha Mngereza, wamesema ni pigo kubwa katika tasnia ya sanaa nchini.

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' wametumia kurasa za mitandao ya kijamii kumuelezea Mngereza na mchango wake katika sanaa ambao hautasahaulika kamwe.

Akimuelezea Mngereza, Msanii Barnaba Classic amesema kifo hicho ni pigo kwa tasnia na anashindwa kupokea taarifa za kifo hicho,anakosa kabisa nguvu.

"Mzee wangu Mngereza nakuita, Doh, hili ni pigo kwa tasnia aisee, nashindwa kupokea hakika nakosa kabisa nguvu, pole familia nzima na BASATA ,Mungu akufanye mwenye tabasamu daima milele.

"R.I.P ,wasanii hili ni pigo,mzee wetu alikuwa zaidi ya kiongozi.Hapana aisee,Mungu tunashukuru kwa kila jambo, wewe ndo unayejua kila ukubwa wa jambo,"amesema Barnaba.

Kwa upande wake Msanii Nasib Abdull maarufu kwa jina la  Diamond  amesema hivi" Dah,nakosa hata cha kuandika...Mkuu si juzi tu tulikuwa Arusha  ulikuja kutuunga mkono kwenye tour yetu ya Tumewasha na Tigo,leo hii umetangulia, dah!Inshallah,Mwenyezi Mungu akulaze mahala pema,peponi, Amina".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...