Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ( katikati) akingungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi toka kwa aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (kulia) leo jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya.Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ( katikati) akiongea mara baada ya kukabidhiwa ofisi toka kwa aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (kulia) leo jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya.

Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya ofisi . Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ( wa pili toka kushoto) na aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( katikati) ,Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kushoto wa kwanza) Wengine na Naibu Waziri Hussein Bashe ( wa pili toka kulia) na Naibu Katibu Mkuu Prof. Siza Tumbo ( kulia).

WAZIRI wa Kilimo Prof Adolf Mkenda amesema kipaumbele chake ni kuona wakulima wanaongeza tija kwenye uzalishaji wa mazo nchini kwa kutumia eneo dogo kuzalisha mazo mengi zaidi na kukuza uchumi wa kaya na taifa.

Waziri wa Kilimo amesema hayo leo (21.12.2020) wakati akikakabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Kilimo  Japhet Hasunga hafla iliyofanyika makao makuu ya wizara ya Kilimo Mtumba jijini Dodoma .

Hafla ya makabidhiano imefanyika kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Prof. Mkenda kuwa Waziri wa Kilimo katika awamu hii ya pili ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano.

“ Sekta ya kilimo inachangia asilimia 28 ya pato la taifa lakini sekta ndogo ya mazao inachangia asilimia 18 ambapo tija ni ndogo. Tija kwenye kilimo ni ndogo sana wakati theluthi mbili ya watanzania inategemea kilimo kwenye maisha ambapo asilimia karibu 70 imejiali huko” alisema Prof. Mkenda.

Katika salamu zake Mhe. Hasunga amesema anamshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini na kumteua kuongoza wizara ya kilimo kwa miaka miwili ya awamu yake ya kwanza na kuwa alifanya  kazi kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula.

“Nimefanya kazi miaka miwili kama Waziri wa Kilimo, nafurahi  katika kipindi chote cha kwanza cha awamu ya tano nchi imeweza  kujitoshelevu kwa chakula” alisema Hasunga.

Hasunga alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na msukumo wa uongozi wa Rais Magufuli pamoja na wakulima wa Tanzania waliotikia kauli mbiu ya kufanya kazi kwa bidii.

Waziri huyo mstaafu na mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoa wa Songwe aliongeza kusema ataendelea kuwa mwaminifu na kuiomba wizara ya kilimo kutilia mkazo suala la upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu bora, viuatilifu, mbolea na zana bora ili kilimo kikue na kuchangia zaidi kwenye pato la taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alisema atahakikisha sekta ya kilimo inaongeza kuchangia ukuaji wa uchumi toka wa sasa wa asilimia 28 hadi zaidi huku sekta ya kilimo mazao ikitoa mchango mkubwa kwenye upatikanaji wa maligahfi za viwanda.

Katika kuhakikisha sekta ya kilimo inatoa mchango mkubwa kwenye kwenye ukuaji wa uchumi nchi, Prof .Mkenda maetaja mambo makuu manne ambayo ni diara kwake wakati akiongoza Wizara ya Kilimo.

Kwanza kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kutumia eneo dogo kuvuna mazao mengi hivyo taasisi ya utafiti (TARI) na wakala wa mbegu (ASA) wana jukumu la kuongoza kwenye utafiti wa mbegu bora nyingi ili wakulima wazalisha zaidi.

Pili, kusimamia na kuelimisha mbinu bora za uzalishaji (Good agricultural practices) ambapo amelenga kufanya umwagiliaji kwa njia ya matone ukue na kuchangia kwenye uhakika wa chakula ikiwemo upatikanaji wa viutalifu na huduma za ugani kwa karibu zaidi .

Mkakati wa tatu Prof. Mkenda ameutaja kuwa ni upatikanji wa masoko ya uhakika wa mazao ya wakulima kwa kusimamia masoko ya kimkakati na kufanya wakulima wanufaike na jasho lao kwa faida huku nchi ikiwa na uhakika wa chakula na malighafi.

Mwisho Prof Mkenda amesema katika uongozi wake ndani ya wizara ya Kilimo atahakikisha upatikanaji wa mitaji na uwekezaji kwenye kilimo unaluwa rahisi na wenye kunufaisha makundi ya vijana na wawekezaji ambapo atatoa mkazo kwenye upatikanaji wa mitaji kupitia miko yenye riba nafuu toka taasisi za fedha nchini na zile za nje ya nchi.

Ka upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alisema kuwa wizara hiyo inazo changamoto ikiwemo kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa upatikanji wa sukari ambapo wa sasa upungufu ni zaidi ya tani 60,000 kila mwaka na upande wa upatikanaji mafuta ya kula upungufu ni zaidi la tani 365, 000 .

Kusaya alitoa wito kwa viongozi wakuu wa wizara wapya kushirikiana na watumishi ili kuhakikisha lengo la serikali ya awamu ya tano la kufikia hekta milioni moja na laki mbili zinafikiwa na kufanya sekta hiyo ichangie zaidi kwenye ukuaji wa uchumi kwani Tanzania ina eneo la hekta milioni 29 zinazofaa kilimo cha umwagiliaji kati ya hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...