Na Woinde Shizza ,ARUSHA 

CHAMA Cha mawakili Tanganyika (TLS) kimewakutanisha wanataaluma wa anuai  (professional diversity ) 800 kujadili maswala mbalimbali wanayokumbana nayo  ,kujua fursa ,changamoto zilizopo katika taaluma zao haswa kwa upande wa Sheria .

Akizungumza katika mkutano  wa kwanza  wa  anuai za kitaaluma  ulioandaliwa na Chama hicho uliofanyika  mkoani Arusha Jana  Rais wa Chama hicho Dkt.Nshala Rugemeleza alisema kuwa wamekutana kujua fursa zilizopo katika kila taaluma  ,kuangalia ni jinsi gani wanasheria wanaweza kushirikiana na watu wa taaluma mbalimbali nakuweza kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa zaidi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao ili  kuweza kwa pamoja  kuwedadisi fursa zilizopo.

Alisema kuwa  sheria huwezi kufanya peke yako, Kama sheria ilivyo ni vyema ukajua watu wa kada mbalimbali wanafanya kitu gani , maana sheria za nchi yetu zinagusa kada zote na  fani zote lakini mwisho wa siku nijukumu la mwanasheria kutoa tafsiri ya hizo sheria 


"Bunge limeweza kutunga sheria  ambazo  zinagusa karibu fani zote lakini mwisho wa siku mwanasheria ndio anatakiwa atowe mwongozo wa hizo sheria kwa kila kada,Ila watu wa kada hizi wamekuwa wakitaka kutoa tafsiri zao ni vyema watu wakaweza kukutana na kujadili namna gani wanaweza  kashirikiana na wanasheria ,wasanifu wa majengo ,wanahabari ,wahasibu  ili kujenga ushirikiano na kuweza kukuza fursa na kutumia teknolojia za kisasa kuweza kukuza uwanda wa ufanyaji wa kazi" alibainisha Rugemeleza

 Akifungua mkutano huo jaji mstaafu Dkt .Fauz Twaib alisema kuwa mkutano huo utawawezesha wadau hao kushirikiana  kwa pamoja na kuboresha njia bora zaidi za kutoa huduma.

"Kwa Sasa  kumekuwa na wimbi kubwa la mawakili ,wametoka kwenye idadi mawakili  Chini ya elfu moja miaka 10 iliopita na kufikia elfu 10 sasa katika hali ya aina iyo na upya wa mawakili wengi unasababisha changamoto kuwa nyingi Sana ,kwa ujumla kuna matukio mengi zaidi yanaoyoonekana kuonyeshwa Kuna aja ya kuangalia namna gani mawakili wanafanya kazi pamoja na maswala ya ueledi wao wa kufanya kazi"alibainisha Twaib

Akiongelea machapisho mbalimbali aliyoyazindua leo kwa ajili ya wanasheria alisema kuwa yatawasaidia kujua sheria mbalimbali ambazo hawazijui kwani hakuna mwanasheria  ambaye anajua sheria zote papo kwa papo hivyo machapisho hayo yatamsaidia kujua kwa haraka kwani yamefupishwa.

Kwa upande wake wakili mstaafu Dkt Hawa Sinare alisema kuwa machapisho haya ni miongozo mzuri kwa wanasheria haswa wageni kwani itakuwa inawasaidia hata hawa wanasheria wachanga kujua Sheria ambazo walikuwa hawayajui.
 
Pichani kushoto ni Jaji Mstaafu Dkt Fauz Twaib akizindua moja ya chapisho kwa ajili ya kusaidia wanasheria  msaada wa kisheria, kulia ni Rais wa Chama Cha mawakili Tanganyika (TLS) Dkt Nshala Rugemela

Jaji mstaafu  Dkt Fauz Twaib  akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano huo 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...