Leo Ubalozi kwa kushirikiana na Makampuni (17)  ya kusafirisha Watalii wa daraja la juu (High-end tourists) ya China umezindua programu maalum ya "Post-card" kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania katika soko la China. Miongoni mwa makampuni hayo ilikuwepoChina International Travel Services (CITS)  inayoongoza katika usafirishaji wa watalii nje ya Nchi.

Kupitia pgm hiyo, "post-cards" zimesainiwa na Balozi na  Mwakilishi wa Ethiopian Airlines na kesho zitapelekwa Tanzania na Shirika hilo ambapo wawakilishi wa Makampuni hayo (17) watapanda Mlima Kilimanjaro hadi kufikia kileleni tarehe 1 Januari 2021 na kupiga picha na "post-cards" hizo

Post-cards hizo zitarejeshwa nchini China na kugawiwa kwa wateja  (premiere customers) 4000  wa Makampuni hayo (17) wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina utakaoadhimishwa kuanzia tarehe 11-17 Februari 2021.

Programu hiyo mbali na kuitangaza nchi yetu katika soko la China, itawezesha Makampuni ya Utalii yanayoshiriki kuonesha upendo na kujali wateja wao ambao katika kipindi cha Mwaka 2020 hawajaweza kusafiri nje ya China kwasababu ya janga la COVID19.  

Aidha, kitendo cha "post-card" kuweza kupandishwa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro siku ya tarehe 1 Januari 2021 kitatoa matumaini kwa wateja wao kwamba mwaka mpya utakuwa ni wa baraka na wataweza kufika kilele cha matarajio na mipango yao kwa mwaka 2021 ikiwa ni pamoja  na kusafiri nje ya nchi baada ya kukaa ndani mwaka mzima.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...