Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 102.5 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi 14 ikiwa ni asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani.

***************************************

 
NA TIGANYA VINCENT
VIKUNDI 14 vya Wajasiriamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui vimepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 102.5 ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji Hemed Magaro wakati wa sherehe fupi ya kukabidhi mikopo hiyo kwa vikundi hivyo.

Alisema kati ya vikundi hivyo 9 ni vya wanawake ambavyo vimekopeshwa kiasi cha shilingi milioni 65 na vikundi 5 vya vijana vimekopeshwa shilingi milioni 37.5.

Magaro alisema hadi hivi sasa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha wameshatoa kiasi cha shilingi milioni 85.6 ambayo ni sawa na asilimia 42 ya kiasi cha shilingi milioni 202.7 ambazo zinatakiwa kukopesha kwa vikundi vya walemavu, vijana na wanawake.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuna madeni ya jumla ya shilingi 170.9 zinadaiwa kwa wakopaji ambapo kati ya hizo vikundi vya wanawake vinadaiwa shilingi milioni 58.4, vijana wanadaiwa shilingi milioni 96.2 na watu wenye ulemavu wanadaiwa milioni 16.2.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati aliitaka Halmashauri hiyo kuanza utoaji wa mikopo ya fedha nyingi na vifaa na zana mbalimbali ambazo zitawasaidia wananchi kuanzisha viwanda vidogo.

“Ifikie kipindi muanze kutoa mashine ili wananchi waweze kuwa na miradi mikubwa ambayo itaharakisha maendeleo” alisema

Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwepo na matokeo makubwa katika maisha ya wananchi kutokana na aina ya mikopo waliyokopeshwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakopeshaji kurejesha mikopo ili iweze kuwasaidia wengine kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...