Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Prof.Augustine Massawe (kulia) akielezea jinsi vifaa vya kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vinavyofanya kazi wakati wa harambee ya kuchangia watoto njiti vifaa na maktaba kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyoandaliwa na Jacquiline Mengi kushirikiana na washika taji la miss Tanzania ijulikanayo kama Beauty Legacy. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mamiss wakifanya mnada wakati wa harambee ya kuchangia watoto njiti vifaa na maktaba kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyoandaliwa na Jacquiline Mengi kushirikiana na washika taji la miss Tanzania ijulikanayo kama Beauty Legacy. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mjasiriamali na Mwanzilishi wa Dkt.Ntuyabaliwe Foundation, Bi Jaqueline Mengi (kulia) akipozi na Nancy Sumari mara baada ya kumkabidhi tuzo ya kuthamini mchango wake kwenye jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...