Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maduka ya TECNO na kurasa
mbalimbali za mtandaoni, watumiaji hao wamekiri kuwa CAMON 16 imekata kiu yao
ya kile walichokuwa wanakihitaji siku zote kutokana na kuridhishwa na ufanisi
wa sifa za simu hiyo hasa upande wa kamera na memori, skrini pamoja na sifa
nyinginezo.

Kulia ni msimamizi wa duka la TECNO mara baada ya kumkabidhi zawadi mteja wa CAMON 16 Bwana Junior Bernard (kulia).
“Hii simu naifurahia sana maana kamera yake sio ya kitoto ni level nyingine kabisa ya ulimwengu wa kamera za simu, ni simu ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kupiga picha nyakati zote hata usiku kwakweli hapa naona pesa yangu imeenda kihalali.” Alisema Junior Bernard
Kwa upande wa watumiaji wengine wameelezea kuhusu CAMON 16 kuwa
imewaondolea kikwazo cha kupiga picha nyakati za usiku na sasa wanaweza kupiga
picha wakati wowote na mahali popote na kwamba ina uwezo hata wa kupiga picha
za vitu vidogo kabisa mithili ya wadudu wadogo au maua madogo. 
Kulia ni msimamizi wa duka la TECNO mara baada ya kumkabidhi zawadi Mariam Juma, mteja wa CAMON 16
“Simu hii ya CAMON 16 imemaliza
kabisa tatizo la kupiga picha usiku, unajua sisi wengine tunapenda sana
kusafiri, na ukisafiri lazima upige picha za ukumbusho, sasa unapokuwa na simu kama
hii picha unachukua vizuri kabisa usiku na kwenye mwanga mdogo picha inatoka
vizuri sana” Alisema Mariam
Juma.
Kushoto ni mteja wa CAMON 16 Bw. Edward Mkuya akikabidhiwa
zawadi na msimamizi wa duka la TECNO mara baada ya kununua simu hiyo.
“Uzuri wa simu hii ya TECNO CAMON 16 ni kwamba kamera yake inakupa
hamasa ya kupiga picha nyingi kwasababu ni nzuri. Lakini nafurahia kwasababu
nikishapiga picha kuna nafasi kubwa ya kutosha kwenye simu kwahiyo siwezi
kuzifuta picha zangu memori ya GB 128 kwa RAM GB 8 sio mchezo” Alisema Edward Mkuya.
TECNO ambayo ni kampuni ya simu kinara Tanzania tayari imeshasambaza CAMON 16 nchini kote na inapatikana nchi nzima ikiwemo kwenye maduka makubwa ya TECNO maarufu Samarthub na pia kwenye maduka ya wauzaji wa simu nchini kote.
Taarifa zaidi unaweza kutembelea ukurasa wa instagram “tecnomobiletanzania” au bofya link hii: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...