Wawekezaji
kutoka nchini Uturuki wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea
fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini ili waweze kuwekeza na
kukuza Diplomasia ya Uchumi baina ya mataifa hayo.
Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo amethibisha
kuwasili kwa wawekezaji hao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki
"Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa wawekezaji
watano kati ya kumi wamefika nchini na kujumika na waturuki wengine
wanaofanya biashara zao hapa nchini.
"Wawekezaji hawa kutoka
Uturuki wamekuja na wamefungua taasisi yao inayojulikana kwa jina la
"Compass Partners" ili kuendeleza biashara na tunaamini kwa kutekeleza
biashara hii tunaenda kuendeleza uchumi wa Tanzania na kutengeneza ajira
kwa watanzania," Amesema Prof. Kiondo
Prof. Kiondo ameongeza
kuwa, hatua ya kwanza wawekezaji hao wameleta bidhaa mbalimbali ili
watanzania wazione, hatua ya pili itakuwa ni uwekezaji wa kiwanda hapa
nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa hapa
nchini.
Aidha, kwa upande wa bidha zinazozalishwa hapa nchini
ambazo zina fursa ya kuuzwa Uturuki ni pamoja na chai, pamba, tumbaku na
kahawa bidhaa hizi zote zina soko kubwa sana nchini Uturuki.
Tunazalisha
tani 350,000 za pamba lakini tunaweza kuchakata asilimia 15 tu, hivyo
tumepata tayari mwekezaji ambaye atawekeza katika kiwanda cha nguo
mkonani simiyu ili kuongeza thamani ya bidhaa ya pamba hapa nchini.
Balozi,
Prof. Kiondo ametoa wito kwa Watanzania kuanza kuchangamkia fursa hizo
za biashara ili waweze kuongeza kipato na kuongeza biashara zao.
Kwa
upande wake, Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah amesema
kuwa biashara kati ya Tanzania na Uturiki imekuwa ikiimarika kila
wakati kwani Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na kufanya biashara.
"Kupitia
uwekezaji katika sekta mbalimbali ni imani yangu kuwa tutaendelea
kukuza na kuimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia," Amesema Mhe. Yah
Aidha,
amewataka Waturuki na Watanzania kutumia fursa za biashara
zinazopatikana baina ya mataifa hayo ili kufanya biashara na kukuza
uchumi wao.
Ushirikiano wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu,
pamoja na mambo mengine uhusiano huo umekuwa ukijikita zaidi katika
kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii hasa katika kutangaza
vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki.
![](https://1.bp.blogspot.com/-YyK081D4T8A/X9jQDzo5gNI/AAAAAAACTx8/decS-Sqm85AEMgaxbb2zqC0w0AxKE9FeACLcBGAsYHQ/w640-h472/1.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...