Na Jane Edward, Michuzi TV Arusha

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ametoa miezi mitatu hadi kufikia machi  31 mwakani kwa mkandarasi wa mradi wa kituo cha kupoozea umeme cha  Lemugur kata ya Mateves mkoani  Arusha kuhakikisha unakamilika ndani ya miezi mitatu kwani upo  nje ya wakati.

Waziri ametoa maagizo hayo leo wakati alipotembelea kituo hicho na kujionea  mwendelezo wake ambao amesema bado hauridhishi kwani wapo nje ya muda kwani kilitakiwa kukamilika desemba mwaka huu.

Pia Waziri  Kalemani amepiga marufuku  kwa Meneja wa Tanesco  Kanda ya kaskazini,mkoa  na wilaya  kutokwenda  likizo ya sikukuu na mwaka mpya badala yake sikukuu yao waifanyae katika eneo hilo la mradi hadi wahakikishe kazi hiyo inaridhisha katika kiwango kinachotakiwa.

Waziri alitoa siku tatu  kwa Meneja mradi msimamizi wa Tanesco ,Timothy Mgaya na Mhandisi mradi msimamizi wa Tanesco ,Blandina Joachim  kutoa maelezo kwa nini mradi huo umesimama na hakuna wafanyakazi na endapo hataridhishwa na maelezo hayo watatolewa kwenye kitengo hicho na kupewa watu wengine wenye uwezo wa kusimamia .

Aidha Waziri alisema kuwa,hajaridhishwa na kasi ya  mradi wa kituo hicho  jinsi unavyoenda kwani mradi ulitakiwa kukamilika desemba mwaka huu lakini hadi sasa hivi umekamilika kwa asilimia 46 kitendo ambacho hakiridhishi.

Naye Mhandisi mradi msimamizi kutoka Tanesco ,Blandina Joachim akijibu hoja hizo za kucheleweshwa kwa mradi alisema kuwa, changamoto kubwa ni vifaa vya mradi huo ambavyo vinatoka nje ya nchi na kuwa vimechelewa kufika kutokana na ugonjwa wa COVID 19 .

Meneja mradi Mkandarasi ,Irfan Dolgic alisema kuwa,wameshindwa kumaliza mradi huo kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali lakini watajitahidi kumaliza kwa wakati kulingana na maagizo ya Waziri.

Waziri Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wakandarasi wa mradi wa umeme katika Kata ya Matevesi(Picha na Jane Edward, Arusha)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...