WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametuma salaam za rambirambi kutokana na kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group, Bw. Subhash Patel kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.

 

“Hayati Shubash, ana mchango wake kwenye sekta ya viwanda, alikuwa rafiki wa wote, mcheshi, ametoa msaada kwa maskini na matajiri na hakuwa mbaguzi,” amesema Waziri Mkuu wakati akimuelezea Bw. Patel.

 

“Ninatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na wote walioguswa na msiba huu. Taifa limempoteza mmoja wa wazalendo wake. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

 

Katika salamu alizozitoa leo (Jumanne, Desemba 15, 2020), Waziri Mkuu amesema amehuzunishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) na mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

 

Mmoja wa wanafamilia amesema, Bw. Patel amefia nyumbani kwake, Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu na anatarajiwa kuzikwa keshokutwa (Alhamisi, Desemba 17, 2020) kwenye makaburi ya Wahindu yaliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam.

 

Mfanyabiashara huyo maarufu nchini alikuwa akimiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa za plastiki, saruji, mabati, nondo, nyaya za umeme, vinywaji, rangi na pia alimiliki hoteli za White Sands na Sea Cliff, Pearlsun Hotel & Resorts.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...