Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Juliana Chipanjilo Mtumishi wa Wizara ya Kilimo nyuma ya Waziri ni Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020 wakati ambapo Mawaziri hao walipokelewa rasmi Wizarani baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 9 Desemba, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma; Tangu wakati huo walianza mara moja kutekeleza majukumu yao katika mikoa tofauti Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakijadiliana jambo kwa mara ya kwanza katika Ofisi ya Waziri katika majengo ya Wizara ya Kilimo Mtumba Mji wa Serikali mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020. Mawaziri hao waliapiashwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 9 Desemba, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Tangu wakati huo walianza mara moja kutekeleza majukumu yao katika mikoa tofauti.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilmo Gerald Kusaya akisoma taarifa maalum ya Wizara wakati wa hafla ya kuwakaribisha rasmi Wizara ya Kilimo; Waziri Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu wake Mhe.Hussein Bashe mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakifuatilia utambulisho kutoka kwa Wakuu wa idara/ Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo leo tarehe 21 Desemba, 2020 mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara Mtumba Mji wa Serikali.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiwahutubia Wakuu wa idara/ Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo leo tarehe 21 Desemba, 2020 mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara Mtumba Mji wa Serikali.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiwahutubia Wakuu wa idara/ Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo leo tarehe 21 Desemba, 2020 mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara Mtumba Mji wa Serikali.

*************************************************

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo mchana tarehe 21 Desemba, 2020 amepokelewa rasmi Wizara ya Kilimo katika Ofisi za Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba na kutoa wito kwa Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi kufikia kuongeza tija kwenye Sekta ya Kilimo Mazao hususan zao la ngano na mazao mengine ya biashara.

Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda ambaye aliambatana na Msaidizi wake; Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe wote kwa pamoja leo wamepokelewa rasmi na Watumishi wa Wizara ya Kilimo katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma na wote kwa pamoja wamesisitiza na kuomba ushirikiano ili kuifaya Wizara ya Kilimo kuongeza tija kwenye mazao ya kilimo.

Katika hafla hiyo ya mapokezi wote kwa pamoja; Walipata nafasi ya kuongea na Menejimenti ya Wizara ambapo Waziri Mkenda amesema Wizara inajukumu kubwa la kuhakikisha taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula pamoja na kufanya Sekta ya Kilimo Mazao inachangia mara dufu katika pato la taifa.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa tija kwenye kilimo bado ipo chini na kuongeza kuwa mazao yanachangia asilimia 18 ya pato la taifa wakati Sekta ya Kilimo kwa ujumla inachangia takribani asilimia 28.2 ya pato la taifa, asilimia 58 ya ajira na asilimia 65.5 ya malighafi inayotumika katika Sekta ya Viwanda, asilimia 28.2 ya pato la taifa na asilimia 30 ya mapato ya fedha za kigeni.

“Ukiangalia zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wameajiriwa kwenye Sekta ya Kilimo; Jambo hili ni lazima tulifanyie kazi kwa ukaribu na kuleta mapinduzi ya kweli. Nchi zilizoendelea unakuta asilimia tano tu (5%) ndiyo wameajiliwa maana yake ni kuwa tija ipo chini, unatakiwa kuwa na idadi ndogo na wengine wajikite kwenye Sekta nyingine”. Amesisitiza Waziri Mkenda.

Naye Naibu Waziri Bashe amesema ili Wizara ifikie malengo yalikusudiwa ni vyema Viongozi pamoja na Watumishi wote wa Wizara kubadili fikra.

Nawapongeza kwanza kwa kuwa tulishirikiana na

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo amesema amemuahidi kumpa ushirikiano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...