Ghala linalomilikiwa na AKHTAR INTERPRISES ambalo limehifadhi mchele mbovu upatao tani 112 unaotarajiwa kwenda kuangamizwa katika jaa la kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar                

JUMLA ya tani 112 za mchele wa basmati zimeteketezwa na mamlaka ya udhibiti na usalama wa dawa na chakula baada ya kukamatwa katika ghala la Akhtar interprises maarufu simba chai liliopo Mombasa nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Tani hizo zimeteketezwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa umepitwa na muda kwa matumizi ya binadamu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa ZFDA Dkt Khamis Ali Omar wakati akitoa maelezo kuhusiana na kuteketezwa kwa mchele huo.

Amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kugundulika kuwa mmiliki wa ghala hilo anatoa mchele kwenye vifungashio vilivyomaliza muda wake tokea 2019 na kungiza   katika vifungashio vipya ambapo utatumika mpaka 2022 jambo ambalo linahatarisha afya ya mlaji.

‘’tunasikitishwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu katika  kuzibadilisha   bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi na kuziingiza katika vifungashio vipya bila ya kujali afya ya watumiaji.’’ Alisema mkurugenzi huyo.

AidhaDkt Khamis amesema ndani ya ghala hilo wamegundua tambi ambazo zishapitwa na wakati pamoja na vifuko vitupu vilivyobadilishwa mwaka kwa ajili ya kuzifunga upya ili kuanza kusambaza  katika maduka mbalimbali.

Hata hivyo Mkurugenzi amesema kwa sasa mmiliki wa Ghala hilo tayari ameshafikishwa katika vyombo vya sheri a kwa hatua zaidi.

Nae Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula ZFDA Suleiman Akida Ramadhan ameta wito kwa wananchi kuangalia na kuzichunguza kwa makini wakati wanaponunua bidhaa zao iwapo watakugundua kuna hitilafu yeyote kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika. 

Aidha amesema ZFDA itahakikisha inaendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa ambazo zipo sokoni ili kuziondosha bidhaa zilizomaliza muda kwa matumizi ya binaadamu.Mkuu wa ukaguzi wa chakula ZFDA Suleiman Akida Ramadhan akitoa ufafanuzi juu ya kugundulika kwa mchele uliomaliza muda kwa matumizi ya binaadamu katika ghala linalomlikiwa na AKHTAR INTERPRISES maarufu SIMBA CHAI huko kibele.Mkurugenzi wa ZFDA Dkt Khamis Ali Omar akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kuteketeza mchele katika jaa la kibele.

Kijikolikiangamiza mchele kwa  kuuchanganya mchele na takataka ambao umemaliza muda wake kwa matumizi ya binaadamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...