Mwaka 2020 karibia unafikia ukingoni, bila shaka mwaka huu umekuwa ni mwaka wa changamoto nyingi kwa duniani nzima, lakini pamoja na hayo mwaka 2020 ni mwaka ambao umefanya teknolojia kutumiwa na watu wengi sana duniani ikiwa pamoja na ujio wa bidhaa bora ambazo zimerahisha maisha ya wengi.
Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha sifa pamoja na ubora wa simu mpya za TECNO zilizotoka kwa mwaka 2020. Kama ulikuwa unafikiria kununua simu ya yoyote ya TECNO iliyotoka mwaka 2020 basi pengine list hii inaweza kusaidia kufanya manunuzi kulingana mahitaji yako.
TECNO Camon 16 Premier
Kama unatafuta simu ya TECNO yenye ubora karibia kila mahali TECNO Camon 16 Premier ni simu bora sana, simu hii inakuja na kamera bora huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na nyingine zikiwa na Megapixel 8 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja ambazo ni low-light sensor. Kamera hizi zinakuja na teknolojia ya image stabilization ambayo inakusaidia kuchukua video za 4K zilizotulia zaidi. Mbali na hayo simu hii pia inao uwezo mkubwa wa kuchukua picha na video bora sana hata wakati wa usiku.

Kwa upande wa kamera ya mbele Camon 16 Premier inakuja na kamera mbili za selfie, kamera moja inakuja na Megapixel 48 ambayo ni wide sensor na nyingine ni Megapixel 8 ambayo hii ni ultrawide. Kamera hizi zote kwa pamoja zina kuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p.

TECNO Camin 16s

TECNO Camon 16s ni toleo lingine la simu mpya za Camon 16 mwaka 2020, toleo hili ni tofauti kidogo na toleo la Camon 16 Premier, kwani kwa bei nafuu zaidi utapata simu hii yenye kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48, kwa kutumia simu hii unaweza kuchukua video hadi za 1080p@30fps. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 8 huku nayo ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

TECNO Camon 15 Premier
Camon 15 Premier ni toleo jingine la simu za Camon, simu hii imetoka mapema mwaka 2020 na inakuja na sifa bora, Camon 15 Premier ni simu inakuja na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 128 huku ikiwa na kamera kuu yenye uwezo wa Megapixel 64 na kamera ya selfie ikiwa na Megapixel 32.

TECNO Camon 15

Camon 15 ni toleo jingine la ambalo pia linakuja na sifa nzuri ikiwa pamoja na kamera kuu ya megapixel 48, pamoja na kamera ya nyuma ya selfie ya Megaixel 16. Kama unataka kuiliki simu ya Camon 15 yenye kamera nzuri basi unaweza kununua simu hii ya Camon 15.

TECNO Pouvoir 4
TECNO Pouvoir 4 ni simu nyingine bora kutoka kampuni ya TECNO iliyotoka mwaka 2020, simu hii ni bora hasa kama wewe unataka simu yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu, simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 amh, battery ambayo inaweza kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi yako.

TECNO Pouvoir 4 Pro

TECNO Pouvoir 4 Pro ni toleo lingine ambalo linakuja na uwezo mkubwa wa battery lakini zaidi ya hapo simu hii pia inakuja na sifa nzuri kama uhifadhi wa ndani wa GB 128 pamoja na RAM ya GB 6. Kama unataka uwezo zaidi na simu yenye kudumu na chaji zaidi basi simu hii ya TECNO Pouvoir 4 Pro ni simu bora kwako.

TECNO Spark 5 Pro
TECNO Spark 5 Pro ni simu nyingine kutoka TECNO iliyotoka mwaka 2020, simu hii inakuja na kioo kikubwa cha Inch 6.6 ambacho kina resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels. Mbali ya kuwa simu hii inayo kioo kikubwa pia inakuja na battery bora yenye uwezo wa kudumu na chaji. Bila kusahau Spark 5 Pro inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja na nyingine ikiwa ni QVGA.

TECNO Spark 5
TECNO Spark 5 ni toleo lingine la Spark 5 Pro, simu hii nayo ni moja kati ya simu ambayo inapatikana kwa bei nafuu zaidi huku ikiwa na kioo kikubwa kama cha Spark 5 Pro cha inch 6.6, pamoja na battery kubwa ya 5000 mAh. Pia simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 na moja ya mwisho ikiwa ni QVGA. Simu hii pia ina uwezo wa resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels.

Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/ kwa mengi zaidi kuhusiana na bidhaa za TECNO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...