Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar akinywa
maji yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa akiwa
sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akiwa na wadau
mbalimbali wanaokuwanywa maji hapoBalozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Akizungumza
wakati alipotembelea banda la maji ya kunywa la kiwanda cha Mkwawa
wakati wa maonyesho ya kibiashara ya mkoani Iringa yaliyofanyika katika
chuo cha Mkwawa balozi David Concar alisema kuwa amepongeza uzalishaji bora wa maji hayo ambayo yamekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa afya ya binadamu.
Balozi
Concar alisema kuwa amekunywa maji hayo na kugundua kuwa yanaradha ya
maji hayo ambayo anaamini kuwa kila mtu atayeonja maji hayo lazima
avutiwe kwa namna yalivyokuwa bora.
Alisema
kuwa amevutiwa na bidhaa hiyo ya maji ya kunywa ya kampuni ya Mkwawa na
kuahidi kuitangaza kokote Kule atakapokuwa ametembea kutoka na kuvutiwa
na jinsi ya uzalishwaji wake ulivyokuwa na bora wa kimataifa.
Balozi
Concar aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho cha uzalishaji wa maji
kuhakikisha wanatanua na kijitangaza zaidi kitaifa na kimataifa kwa
sababu ametembea kwenye super market nyingi hajaona maji ya kampuni hiyo
ambayo yeye anaamni kuwa in maji bora hapa nchini.
Akiwa
ameambatana na balozi wa uingereza nchini Tanzania, mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela alisema kuwa amekuwa balozi wa kujitegemea
kuyatangaza maji hayo kila kona ya Tanzania kutokana na ubora wake.
Alisema
kuwa anamuomba balozi huyo Nate awe balozi wa kutangaza maji
yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kutokana na ubora wake ambao maji
hayo yanayo.
Kasesela
aliwataka viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatanua wigo wa
masoko ya bidhaa hiyo ya maji ya kampuni ya uzalishaji wa maji ya Mkwawa
inayopatikana mkoani Iringa wilaya ya Iringa.
Alisisitiza
wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kuendelea kunywa
maji safi na salama yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo
mkoani Iringa kutokana na ubora wake.
Kwa
upande wao baadhi ya wanachi mkoani Iringa waliohudhulia katika
maonyesho hayo yaliyofanyikia katika chuo cha Mkwawa waliyapongeza maji
hayo safi na salama kwa kunywa kutokana na ubora wake.
Walisisistiza
kuwa wataendelea kunywa maji hayo yaliyokuwa na ubora wa hali ya juu
lakini wanatakiwa kuhakikisha wanaulinda na kuuboresha ubora wake ambao
upo hadi hivi sasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...