Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni ya Wasafi Tv kutoa huduma kwa muda wa miezi 6 kuanzia January 6 mwaka huu hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza utupu kinyume na kanuni za maadili katika tamasha la Tumewasha Live Concert lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...