Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akizindua Katiba ya jumuiya ya wahitimu ya chuo cha Ufundi Arusha(ATC Alumni association.)


Jane Edward, Michuzi TV- Arusha

MKUU wa Wilaya ya Hai Lengai ole sabaya amepongeza bunifu zilizofanywa na chuo cha Ufundi Arusha(Arusha technical College) kwa matumizi ya  teknolojia zinazotumia dhana rafiki 

Sabaya aliyasema hayo wakati akizindua umoja wa wanafunzi waliosoma katika chuo cha ufundi Arusha wenye lengo la kuendeleza ugunduzi walioufanya pamoja na kusaidia wanafunzi waliopo kujifunza juu ya teknolojia za kisasa na baadaye kusaidia jamii inayowazunguka.

"zipo mamlaka ndani ya serikali zinashindwa kuwapa nafasi wanachuo wanaoonyesha bunifu zao ,hali ambayo inasababisha nchi kutokuwa na vijana wazawa wenye uwezo wa kulitumikia Taifa." alisema Sabaya.

Alioongeza kuwa, ni kazi ya serikali kubeba vijana bunifu wanaoonyesha moyo na utayari katika mambo ya msingi ikiwemo vifaa ambavyo vimebuniwa na vijana wa chuo hicho cha ufundi ambavyo vinawezesha kutatua changamoto mbalimbali.

Sabaya alisema  kuwa,ni vyema Nacte na TCU wakakaa pamoja na kuunda bodi moja itakayosaidia vijana wabunifu kufanikisha ugunduzi wao na sio kila mmoja kuwa na vigezo vyake kwani jambo hilo linawarudisha nyuma na kuwakatisha tamaa na kufanya jamii kuendelea kuamini teknolojia za  nje.

Mkurugenzi wa elimu ya ufundi kutoka wizara ya elimu, Dokta Noel Mbonde  alisema kuwa,ni vyema wanafunzi wanapohitimu chuo wakaendeleza kwa vitendo kile alichokipata kutoka chuoni hapo ili kuonyesha umuhimu wa uwepo wao.

 "kitendo cha kuondoka huna chochote ulichokipata chuoni hautakuwa na msaada katika Taifa hili, hivyo natoa rai kujiendeleza na mwishowe kufikia nafasi za juu za uongozi kwani sisi tunapita hivyo mjitahidi nakuacha kujidharau nyie wenyewe kwani serikali hii inajali vijana,"alisema  Dkt Noel.

Aliongeza  kuwa, ni vyema vijana wasitegemee  kuajiriwa bali wajiandae kujiajiri na kwa kufanya hivyo ni lazima wahakikishe wanaigeuza elimu walioipata kuwa ya vitendo zaidi.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho cha Ufundi,Issa Suleiman    alisema kupitia umoja huo wanafunzi waliomaliza kwenye chuo hicho utasaidia kubadilishana uzoefu na ubunifu mbalimbali walionao lakini changamoto wanayopata ni upatikanaji wa fedha ili kuendeleza taaluma yao.

"Kilichopelekea  kuzindua  jumuiya hii ambayo itasaidia kupata fedha na kuangalia mpangilio wa fedha utakao enda kuendeleza ubunifu unaofanywa na baadhi ya wanafunzi ili kuachana na dhana ya kuuza wazo bali waweze kutengeneza bidhaa zao kamili,"alisema rais huyo.

Uzinduzi wa jumuiya hiyo ya wanafunzi waliomaliza chuo cha Ufundi Arusha, unatajwa kuwa na manufaa ya kuwafanya wahitimu hao kurudi chuoni na kutatua changamoto zinazoikabili chuo hicho katika nyanja mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...