Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo wakati wa kufunga kikao cha Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi   

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akifunga kikao cha Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati wa kikao cha utendaji wa Shirika hilo kilichofanyika Dodoma. Anayesikiliza kwa makini ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akifafanua jambo wakati wa kufunga kikao cha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) na Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Menejimenti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na wawakilishi wa taasisi za Wizara hiyo wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wa mikoa yote kilichofanyika Dodoma

Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wa mikoa yote wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha Mameneja hao kilichofanyika Dodoma

Meneja Kituo cha Biashara Pemba wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Khamis Ngwale akimshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula kwa niaba ya Mameneja wa Shirika hilo baada ya kutoa neno la shukrani kwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto) baada ya kufunga kikao cha Mameneja hao, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi.

======  =========  =========  ==========

à        TTCL Kuongeza Idadi ya Wateja kutoka Asilimia 2 hadi 6 kwa Mwaka

à        Kuongeza Idadi ya Mawakala wa Vocha, T - PESA kutoka 2,800 hadi 3,080

à        Chukueni Hatua kwa Wahujumu wa Miundombinu ya TEHAMA

à        Kuongeza Ubunifu na Utafiti wa Masoko ya Huduma na Bidhaa za TTCL

à        Boresheni Mifumo ya Huduma kwa Wateja

à        Kuingiza Mkataba na Mkurugenzi Mkuu, Mameneja Kupima Utendaji Kazi

à        Kata Huduma kwa Taasisi za Umma Zinazodaiwa na TTCL

à         Angalieni Upya Mikataba Inayogharimu Uendeshaji wa TTCL

 

Na Prisca Ulomi,WMTH

 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amefunga kikao cha Mameneja wa Mikoa yote ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kilichofanyika Dodoma kwa muda wa siku tatu ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi, Menejimenti ya Wizara na wa TTCL na wawakilishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo

 Dkt. Ndugulile ameipongeza TTCL kwa kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kuazimia kuongeza idadi ya wateja kutoka asilimia 2 hadi asilimia 6 kwa mwaka mmoja wanaotumia simu za mkononi waliopo kwenye soko; kuongeza idadi ya mawakala wa vocha na wa huduma za fedha mtandao za T – PESA kutoka 2,800 hadi 3,080 katika kipindi cha miezi mitatu; na kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wateja

 Amesema kuwa imejitokeza tabia ya baadhi ya taasisi za umma kutumia huduma za TTCL bila kulipa na amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba kuziandikia taasisi zinazodaiwa kuwa walipe madeni yao vinginevyo ifikapo tarehe 31 Januari, 2021 wazikatie huduma hizo  

 Ameilekeza TTCL kuchukua hatua kwa watu wanaohujumu miundombinu ya TEHAMA ya TTCL na kudhoofisha ubora wa huduma zake; kuboresha mifumo ya kuhudumia wateja ili kuongeza imani ya wateja kwa Shirika; kuangalia upya mikataba inayoigharimu Shirika ambayo imesainiwa baina ya TTCL na watoa huduma; wajiandae kuingia mikataba baina ya Wizara na Mkurugenzi Mkuu wao na Mameneja ili kupima utendaji kazi; na waongeze ubunifu na kufanya utafiti wa masoko ya huudma za bidhaa zinazotakiwa na wateja

 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Wizara na taasisi tukipanga kwa pamoja inakuwa rahisi kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa malengo na maazimio tuliyojiwekea ya kuhudumia wananchi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameikumbusha TTCL kuhakikisha kuwa wanajali mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa TTCL ili kuwaongezea ari, morali na motisha ya kuwahudumia wateja

 Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa wamejipanga kutekeleza maazimio na malengo waliyojiwekea ili kuomgeza huduma na bidhaa za mawasiliano kwa wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...