Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoani Manyara, imemfungulia mashtaka ya jinai Dunga Othman kwa kujipatia shilingi milioni 58.4 kwa njia za udanganyifu kwa wakulima watatu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Makungu amesema kesi hiyo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu namba CC.1/2021 ipo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara, Simon Kobelo.

Amesema kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo na waendesha mashtaka wawili wa TAKUKURU, mawakili Evelyne Onditi na Martini Makani.

Amesema hati ya wito kwa mshtakiwa imetolewa na mahakamani, ambapo Dunga afahamu pia analazimika kufika kama ilivyoelekezwa kwenye wito huo.

“Na endapo atakaidi wito huo utaratibu mwingine wa kumfikisha mahakamani hapo kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, utafuatwa,” amesema Makungu.

Amesema uchunguzi dhidi ya Dunga umekamilika na unaonyesha kuwa mshtakiwa alipokea jumla ya shilingi milioni 58.4 kwa njia ya udanganyifu kwa wakulima watatu wa mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang’.

Amesema wakulima hao walikuwa na uhitaji wa matreka ambapo kila mmoja kwa kiwango tofauti kama ilivyofafanuliwa kwenye hati ya mashtaka iliyofikishwa mahakamani.

“Mshtakiwa alijipatia fedha hizo mwaka 2016 kwa kuwashawishi wakulima hao kuwa anatoa huduma ya kukopesha kupitia kampuni aliyoianzisha ya Farm Green Imprements Ltd.” Amesema Makungu.

Amesema hata hivyo baada ya kufanikisha lengo lake Dunga aliua kampuni hiyo kabla ya kuwaletea wakulima hao matreka au kurejesha fedha hizo kwa maelezo kuwa kampuni hiyo ilikufa.

Ametoa rai kwa wenye mawazo ya kujificha kwenye kampuni wanazozianzisha wakiwa na nia ovu ya kudhulumu watanzania walio wanyonge, waache fikra hizo kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai inatambua huo ulaghai na atakayejaribu ataondolewa blanketi la kampuni na kushtakiwa.

“Ifahamike kuwa vitendo vya namna hii hutafsiriwa kama utakatishaji wa fedha na kinyume na kifungu cha sheria ya 12/2016 na wale watakaobainika wanadhulumu watu watawajika kwa mujibu wa sheria hii ya utakatishaji fedha.” Amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...