WAZIRI wa kilimo.Prof.Adolf Mkenda amefanya
mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya uzalishaji wa sukari hapa
nchini.
Prof.Mkenda amesema kuwa uzalishaji
wa sukari hapa nchini umekuwa ukiongezeka katika kipindi cha miaka
mitano uzalishaji wa sukari umeongezeka kwa asilimia 78.3 (kutoka tani 295,775
mwaka 2015/2016 hadi tani 377,527 zinatarajia kuzalishwa msimu wa 2020/2021)
Hata hivyo Prof.Mkenda amesema kuwa mafanikio
haya ya kuongezeka kwa uzalishaji ni matokeo ya utekelezaji wa sera na mikakati
ambayo serikali imeweka kuhakikisha wazalishaji wana mazingira mazuri ya
kufanya upanuzi wa mashamba na wakulima kuongeza tija.
Aidha ,katika msimu wa mwaka 2020/2021 jumla
ya tani 377,527 za sukari zitazalishwa kutoka kwenye viwanda vilivyopo vya
Kilombero Sugar Company Ltd,Mtibwa Sugar
Estate, Kagera Sugar Ltd, TPC Ltd na Manyara Sugar Ltd. Pia amesema kuwa mahitaji ya sukari kwa ujumla
hapa nchini kwa matumizi ya kawaida na viwandani ni tani 655,000 kwa mwaka.
Pof.Mkenda ameendelea kusema kuwa ili kuongeza
uzalishaji Serikali imejipanga kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa
wakulima wadogo, viwanda viongeze uwezo wa kuchakata miwa inayozalishwa na
kuongeza tija kwa uwepo wa mbegu bora na
viuatilifu.
Kutokana na uhaba wa sukari uliopo na miwa ya
wakulima kubaki mashambani bila kuvunwa kwa sababu ya ufanisi na uwezo mdogp wa
viwanda, serikali imeelekeza Kiwanda cha Kilombero na viwanda vingine kuongeza
na kuimarisha uwezo wa uchakataji wa miwa ili kunusuru hasara kubwa wanayoipata
wakulima kwa kutovuniwa miwa yao na kupelekwa kuchakatwa viwandani.Alisema
Prof. Mkenda
Serikali haitosita kuchukua hatua ya kuruhusu
mwekezaji mwingine kujenga kiwanda cha kati kimoja au viwanda vidogo viwili
endapo mwekezaji aliyopo sasa katika bonde la Kilombero atashindwa kufanya
upanuzi unaostahili kwa wakati ili miwa ya wakulima wadogo takribani tani
200,000 inayobaki katika bonde la kilombero ipate soko la uhakika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...