MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA, UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KWA MWAKA 2020 YAMETANGAZWA LEO IJUMAA JANUARI 15,2021.
 
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yakionyesha kuwa asilimia 85 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu.
 
Kwa mujibu wa Necta iliyotangaza matokeo hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 kupitia kwa katibu mtendaji wake, Dk Charles Msonde, watahiniwa 434,654 walifanya mtihani huo na 373, 958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali.
 
Dk Msonde amesema kwa matokeo hayo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 5.19.
Katika mtihani huo Paul Luziga wa sekondari ya Pandahill iliyoko Mbeya amekuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa.
 
TAZAMA MATOKEO HAPA..BOFYA LINK

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...