MBUNGE wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto  Mkoani Tanga, January Makamba amemwomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwasaidia wakulima wa chai wa jimbo hilo kumaliza tatizo la kuendelea kusimama kwa kiwanda cha chai cha Mponde.

January Makamba alitoa ombi hilo katika kikao cha Wadau wa zao la Mkonge kilichofanyika jijini Tanga na kuongozwa na Waziri Mkuu.

Alisema kuwa wakulima wa zao hilo wa chai walifarijika sana wakati Waziri Mkuu alipofanya ziara mahususi kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na walifarijika pia walisikia ahadi za serikali kufungua kiwanda hicho.

Makamba alimwomba Waziri Mkuu asaidie ili kufikia tamati ya tatizo kama ilivyotolewa ahadi na serikali.

Alishauri kuwa kama kuna changamoto zinazozuia uharakishaji wa kufungua kiwanda basi serikali ichukue hatua ya kukaribisha wawekezaji kwa kutangaza tenda ya kuendesha kiwanda hicho.

Akijibu ombi hilo, Waziri Mkuu alimhakikishia Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, Amiri Shehiza kuwa serikali inafuatilia kwa karibu tatizo hilo ili wakulima waweze kuchakata majani maichi ya chai karibu na mashamba yao.

Majaliwa alieleza kuwa serikali ilikuwa na mazungumzo kujua namna bora ya kufufua kiwanda hicho na akaendelea kuwa  serikali imefanya ukaguzi na imeridhia ripoti hiyo.

“Tumezungumza na Shirika la Hifadhi ya Jamii  (NSSF) tumeshauri wawatumie wataalamu wazee wazoefu ili waanze kuwashawasha mitambo wajue wapi kuna matatizo ili yarekebishwe,” Alieleza.

Alisisitiza kuwa nia na malengo ya serikali ya awamu ya tano kuona wakulima wa chai wa Bumbuli wanachakata majani ya chai karibu na mashamba yao.

Wakulima kwa sasa wanalazimika kukata majani hayo na kuyasafirisha hadi kiwanda cha Hekulu ambacho hakina uwezo wakuzalisha majani mengi ya chai.

Kiwanda cha Mponde  kilichofungwa mwaka 2013 baada ya wakulima kugoma kuuza majani yao katika kiwanda hicho ambacho kilikuwa kinaendeshwa na Mwekezaji aliyekuwa ameingia mkataba na Chama cha Wakulima wa Chai (Usambara Tea Growers Association – UTEGA.)

 Kiwanda cha kusindika  majani mabichi  ya chai cha Mponde kilianza kujengwa  mwaka  1969-1970, chini  ya Mamlaka  ya Chai Tanzania (T.T.A), Mnamo  mwaka 1988 kiwanda  hicho  kilibinafsishwa  na kupewa Chama cha Wakulima wa Chai cha Usambara (UTEGA) ambao wamlimtafuta mwekezaji kwa ajili ya kukiendesha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...