Kamati
ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania
(MKURABITA) inaanza ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za
urasimishaji wa ardhi na biashara katika mikoa ya nyanda za juu
kusini.
Akieleza kuhusu ziara hiyo Jijini Dodoma katika
mahojiano maalum yaliyofanyika Januari 23, 2021, Mratibu wa Mpango huo,
CPA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa kamati hiyo itashiriki katika
kazi mbalimbali ikiwemo zoezi la utoaji hati za hakimiliki za kimila za
kumiliki ardhi katika halamshauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na
uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya masjala ya ardhi katika
Kijiji cha Kapya wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Akieleza zaidi
kuhusu ziara hiyo Dkt. Mgembe amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja
inaanza leo Januari 24, 2021 hadi Januari 31,2021.
MKURABITA
imekuwa ikiwezesha wanachi kipitia urasimishaji ardhi na biashara katika
halmashuri mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi
kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Home
HABARI
KAMATI YA UONGOZI MKURABITA YAANZA ZIARA YA UFUATILIAJI NA UTEKELEZAJI SHUGHULI ZA URASIMISHAJI ARDHI NA BIASHARA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...