Mkurugenzi wa kituo cha Uvumbuzi na Ujasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Dkt. Ambrose Itika ambaye alikiwa mgeni rasmi katika kilele
cha utowaji Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student
Entrepreneur awards - GSEA) (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na mshindi wa Tuzo hiyo ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi
kwa mwaka wa kwanza,
Denis David (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Mratibu Mkuu
wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur
awards - GSEA), Emir Karamagi, Rais na Mratibu wa Tuzo za Ujasiriamali
kwa Wanafunzi hapa nchini, Rajabu Katunda pamoja na Mkuu wa Rasilimali
Watu wa Karimjee Jivanjee Group, Janet Lekashingo. Wanafunzi wa vyuo
mbalimbali nchini walishindanishwa katika ubunifu wa ujasiriamali na
Denis David akaibuka mshindi kwa
ubunifu wake wa kuhifadhi mazingira kwa kuokota Nywele katika saluni za
vinyozi mbalimbali na kutengeneza Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea
Viwatilifu vinavyouwa magugu mashambani, ambapo amejipatia kiasi cha
dola za Kimarekazi 1000 (Elfu moja) zitakazomsaidia katika kuendeleza
ubunifu wake.
Mshindi wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza, Denis David akizungmza na kutoa shukrani kwa waandaaji wa tuzo hizo mara baada ya kuibuka Mshindi katika kilele cha mashindano hayo yaliyowakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Denis David kaibuka mshindi kwa ubunifu wake wa kuhifadhi mazingira kwa kuokota Nywele katika saluni za vinyozi mbalimbali na kutengeneza Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea Viwatilifu vinavyouwa magugu mashambani, ambapo amejipatia kiasi cha dola za Kimarekazi 1000 (Elfu moja) zitakazomsaidia katika kuendeleza ubunifu wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Cool Blue Limited akizungumza wakati wa hitimisho la shindano la Global Student Entrepreneur awards (GSEA) lililoshirikisha wanachuo wajasiriamali hapa nchini.
Mshehereshaji Miranda Naiman akizungmza wakati wa hitimisho la Shindano la Global Student Entrepreneur awards (GSEA), lililofanyika jijini Dar es Salaam na Denis David kuibuka Mshindi wa shindano hilo.
Mshindi wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza, Denis David akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake.
Mshindi wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza, Denis David akiwa katika picha ya Pamoja na waandaaji wa shindano la Global Student Entrepreneur awards (GSEA) pamoja na majaji.
========= =========
MSHIRIKI wa shindano la kuwania Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi Ulimwenguni (Global Student Entrepreneur awards - GSEA), David Denis aibuka kidedea katika shindano hilo lililoshirikisha wajasiliamali vijana na wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini.
Shindano hilo lilishindaniwa na wengi lakini tamati ya mashindano hayo walipata washiriki watano ambao ni Upendo Ngusa, Mwaki Mashy, Balbina Gulam, David Denis, Adam Duma ambapo kila mmoja alipata nafasi ya kuelezea wanachokifanya na jinsi walivyoajiri vijana katika miradi wao hiyo.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo Mkurugenzi wa kituo cha Uvumbuzi na Ujasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ambrose Itika alisema kuwa washiriki wa shindano hilo wanatakiwa wajikite zaidi katika ubora wa bidhaa zitakazo saidia jamii zaidi ili kuendelea kulinda mazingira nchini.
"Mmeonesha ujuzi wenu hapa sasa nendeni mkauendeleze ili kuleta matokeo mazuri zaidi na kuleta manufaa katika jamii zetu bila kuharibu amani ya nchi yetu huku mkifanya kazi na watu tofauti tofauti kwa kujiletea faida katika miradi yenu ya maendeleo." Amesema Dkt. Itika
Kwa upande wake Mshindi wa shindano la GSEA na Mkurugenzi wa taasisi ya Cutoff Recycle, Denis David amewashukuru waanzilishi wa Mashindano hayo kwani yamekuwa yakiibua na kuwafunza watu wengine pamoja na kutatua changamoto katika jamii inayowazunguka.
Denis amesema kuwa ushindi huo si wake peke yake bali ni wa kila mfanyakazi wa kampuni yake ya Cutoff Recycle na kwa wale watunza mazingira wote kwa kutumia kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia takataka.
Mshindi wa shindano hilo, Denisi aliyetokea Arusha na Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza amesema kuwa ubunifi wake ni wa kuhifadhi mazingira kwa kuokota Nywele katika saluni za vinyozi mbalimbali Mkoani Arusha na kutengeneza Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea Viwatilifu vinavyouwa magugu mashambani.
"Sisi tunafika kwenye saluni ili kuhakikisha nywele hazitupwi kwenye dampo kwani zitazidi kuongeza uchafu kule baada ya kukusanya nyingi tunazibadilisha zile nywele halisi za bianadamu na kuwa mbolea ya kimiminika." Amesema Denis
Amesema kuwa nywele halisi za binadamu zinaweza kutengeneza viwatilifu ambavyo vinauwa magugu shambani na zimeweza kusaidia kutuza mazingira.
"Tunatengeneza bidhaa ambazo ni rahisi kwa matumizi huku tukizingatia utunzaji wa mazingira kwa kutengeneza bidhaa zinazoweza kutumika tena huku tukiajili kundi la vijana." Amesema Denis
Hata hivyo ameiomba serikali kutembelea wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanaotumia takataka kutengeneza bidhaa nyingine kwa kusaidia kutunza mazingira yetu.
Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ikiwa kwa mwaka 2019/2020 Moses Katala aliibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni Moja. Na mashindano ya 2020/2021 David Denis amejipatia dola za Kimarekazi 1000 (Elfu moja) kwa kuibuka mshindi wa shindano la GSEA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...