Na Woinde Shizza, Michuzi TV-Arusha
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo amepiga marufuku walimu wakuu, wakuu wa Shule, watendaji Kata na Vijiji kuwarudisha nyumbani Wanafunzi ambao Wazazi wao hawajatoa
michango ya Chakula na Katarasi ambayo wamekubaliana kwenye Vikao
kamati za shule, bodi za Shule, Halmashauri za Vijiji na mikutano
mikuu.
Rai hiyo imetolewa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya
wananchi na wazazi kulalamikia vitendo vya wanafunzi kurejeshwa
majumbani kutokana na wazazi wao kutokutoa michango .
Mkongo amesema, Halmashauri hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali za
kinidhamu walimu au watendaji watakaohusika kuwarudisha nyumbani
Wanafunzi kwa sababu za michango kwani kufanya hivyo ni kinyume na
maelekezo ya Waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016.
Mkongo ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano na
Madiwani wa Kata ya Mbuguni na Shambarai Burka, wenyeviti wa vijiji,
wenyeviti wa vitongoji, wajumbe wa Halmashauri za vijiji, watendaji wa
Kata na vijiji, walimu na waratibu Elimu wa Kata hizo uliofanyika
katika ukumbi wa ofisi za Tarafa ya Mbuguni.
Ikumbukwe kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha kwaajili ya utoaji wa
Elimu Bila Malipo katika shule za Sekondari na Msingi katika
Halmashauri ya Meru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...