Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC) Mhe. Seleman Zedi akizungumza katika kikao cha Kamati
kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma, katika kikao hicho kamati
ilipokea maelezo kutoka Hazina kuhusu uhusiano wa Hazina na kamati ya
LAAC.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
wakimsikiliza Kamishna wa Bajeti, Ndugu Balandya Elikana wakati
akiwasilisha maelezo kuhusu uhusiano uliopo kati ya Hazina na Kamati
ya LAAC katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
Kamishna wa Bajeti, Balandya Elikana akiwasilisha maelezo kuhusu
uhusiano uliopo kati ya Hazina na Kamati ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (LAAC) katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni
Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...