MBUNGE wa Kibamba awapatia zawadi wagonjwa Mloganzila.
Mbunge wa jimbo la Kibamba Mhe.Issa Mtemvu amewatembelea wagonjwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kutoa zawadi kwa baadhi ya wagonjwa wenye uhitaji.

Zawadi hizo zimejuisha pampasi za watu wazima, mafuta ya nazi,Maji ya
kunywa,sabuni,miswaki pamoja na dawa za meno.

Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Deogratias Manyama
amemshukuru mbunge huyo kwa kuwatembelea wagonjwa na kutumia fursa hiyo kueleza baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ikiwemo gharama za uendeshaji pamoja na changamoto ya vyombo vya usafiri.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi katika wodi ya wagonjwa wenye
uhitaji hospitalini hapa, Mhe. Issa Mtemvu amesema kuwa lengo la kutembelea
Mloganzila ni kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa na kuwatakia heri ya mwaka mpya.

“Nimekuja kuwapa mkono pole kama mwakilishi wenu bungeni na kuwatakia heri ya mwaka mpya pamoja na kutumia fursa hii kusikiliza changamoto zinazoikabili hospitali hii ili niweze kuziwasilisha bungeni kwa waziri mwenye
dhamana.”amesema Mhe. Mtemvu.

Mhe. Mtemvu amewataka wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa uhakika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...