MKUU wa mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta amempongeza mkuu wa wilaya ya Arumeru na uongozi mzima wa halmashauri ya Meru, na Halmashauri ya Arusha  kwa hatua nzuri waliyofikia katika ujenzi wa madarasa.

Rc Kimanta ambae amefanya ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika halmashauri za Meru na Arusha amesema kasi ya ujenzi inaridhisha na kuwataka kuendelea na kamapani ya ujenzi endelevu wa madarasa katika wilaya ya Arumeru kampeni inayoratibiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri za meru na Arusha Dc pamoja na wenyeviti wa Halmashauri zote mbili na wabunge wa Arumeru mashariki na Arumeru Magharibi.

Rc Kimanta pia amefurahishwa na jitihada za ujenzi wa shule tatu mpya za Faye Crane chemchem ambayo ni ya primary na Shule ya sekondari ya elimu maalum Patandi zote zikiwa za serikali Halmashauri ya meru pamoja na shule ya mchepuo ya Kingereza ya Mringa ambayo inamilikiwa na Halmashauri ya Arusha Dc shule zote ziko katika hatua za mwisho za kukamilika na zitaanza kupokea wanafunzi mwaka huu 2021.

Akitoa taarifa kwa Rc Kimanta, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amesema Mpaka kufikia tarehe 18.01.2021 madarasa jumla ya 30 yatakuwa yamekamilika na kabla ya tarehe 28.02.2021 madarasa 28 yatakuwa yamekamilika na kufikia idadi ya madarasa 58 yanayoitajika kwa msimu huu kutokana na ongezeko kubwa la  wanafunzi wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...