Na. Shukrani Kawogo, Njombe.

Walimu wa shule ya sekondari Chief Kidulile iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe, wametakiwa kuongeza juhudi za kuwafundisha wanafunzi ili kupunguza ama kuondoa kabisa division four zinazojitokeza kwa wingi shuleni hapo na kuinua kiwango cha elimu zaidi.

Hayo ameyasema mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipotembelea shuleni hapo kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu pamoja na wanafunzi na kuzitafutia ufumbuzi wake.

Akipitia matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2018 na 2019 mbunge huyo amesema matoke hayo si yakufurahisha kwani kwa mwaka 2018 hakukuwa na division one yoyote, division two zilikuwa tano, division three nane, division four zikiwa 52 na mwaka 2019 nako hakukuwa na division one, two napo zilikuwa tano, division three 14 huku division four zikiwa 73.

Alisema matokeo hayo si mazuri hata kidogo kwani division four zimekuwa nyingi zaidi kitu ambacho hakileti picha nzuri hivyo amewaomba walimu kufundisha kwa bidii na endapo kutakuwa na changamoto inayohitaji utatuzi wake wasisite kumuambia ili kuondoa vikwazo vitakavyosababisha kushusha ufaulu kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa kuanzia sasa atakuwa ananunua kila alama 'A' itakayopatikana shuleni hapo ambapo atainunua kwa shilingi laki mbili ambayo ataikabidhi katika uongozi wa shule na mwalimu wa somo hilo atapata shilingi elfu hamsini.

"Nawaomba sana mfundishe kwa bidii ili kuinua kiwango cha ufaulu hapa shuleni, najua uwezo wenu wa kufundishia ni mzuri hivyo mimi mbunge wenu nipo tayari kutatua changamoto ambazo zinanihusu na zinaonekana kuwa kikwazo kwenu katika kufaulisha wanafunzi", Alisema Kamonga.

Pia aliwapongeza walimu hao kwa kufanya vizuri kwa kidato cha sita kwa kutoa matoke mazuri ukilinganisha na kidato cha nne ambapo division one zilikuwa tano two nane kwa mwaka 2019.

Aidha kwa upande wa walimu walieleza changamoto mbalimbali zinazowafanya washindwe kufikia malengo ikiwemo kutokuwepo kwa maktaba, vitabu kutokidhi idadi ya wanafunzi, wingi wa wanafunzi kuzidi walimu na sababu nyinginezo ambazo walimu hao walizitaja kuwa ni moja ya kikwazo kwao.

Sanjari na kutembelea shule hiyo pia alifanya mkutano na wananchi wa kata ya Ludewa ili kusikiliza changamoto zao ambapo wananchi hao walieleza changamoto nyingi ikiwemo kuomba kuwekewa mipango miji  ya wilaya katika kijiji cha Ludewa kijijini na kuwawezesha kupewa hati miliki.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mzee mmoja aliyetambulika kwa jina la Cyprian Haule amesema kuwa ardhi ya kijiji chao imekuwa haina thamani ukilinganisha na baadhi ya maeneo kama mdonga ambapo ardhi ya robo heka kwa kijiji hicho inauzwa kwa shilingi laki moja na nusu huku kiwango hicho hicho cha ardhi kwa eneo hilo la mdonga huuzwa milioni moja na laki nane kitu ambacho kinawafanya wajione hawana thamani kwani kutoka Ludewa kijijini mpaka mdonga ni mwendo ambao hata saa moja halifiki.

Hoja hiyo ilimgusa sana mbunge huyo na kumlazimu kumsimamisha Afisa ardhi ili kutolea majibu suala hilo kwani kuwepo kwa mipango miji husaidia kupatikana huduma nyingi za kijamii ikiwemo miundombinu mbalimbali kama barabara, maji, umeme na mingineyo.

"Hakuna kitu muhimu kama mipango miji kwani mipango miji huja na Maendeleo mengi sana hivyo ni vyema afisa ardhi atueleze mipango yao juu ya suala hili",  Alisema Kamonga.

Erick Chigome ni mmoja wa watendaji katika ofisi ya ardhi wilayani humo ambapo alitolea ufafanuzi suala hilo kwa kueleza kuwa awali walishaanza zoezi hilo la upimaji ambapo kukawa na upotoshwaji juu ya zoezi hilo kuwa ni la kitapeli.

Amesema hata hivyo waliwaanzishia hati miliki za kimila ambazo ukomo wake ni kwa njia ya urasimishaji hivyo alimuomba mwenyekiti wa kijiji hicho kuandaa mkutano wa hadhara ili kuweza kuwapa elimu wananchi hao juu ya urasimishaji.

Sambamba na changamoto hizo pia changamoto nyingine ni miundombinu mbalimbali kama umeme, maji, barabara ambapo mbunge huyo amazichukua na kuahidi kuzifanyia kazi.

Mbunge wa jimbo la Ludewa akizungumza na walimu wa shule yasekondari Chief Kidulile iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Mkuu wa shule ya Chief kidulile (wakwanza kulia)akiendelea kumuonysha mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph  Kamonga madarasa ya wanafunzi.
Mbunge wajimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa darasani na wanafunzi wa kidato cha kwanza, katika shule ya sekondari Chef Kidulile iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Waalimu wa shule ya sekondari Chief Kidulile wamsikiliza mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga p(hayupo) pichani alipowatembelea shule hapo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa kushoto, akisikiliza changamoto za wananchi na kuziandika alipofanya mkutano wa hadhara katika kata ya Ludewa mjini.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (hayupo pichani)
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akiwa na mkuu wa shule ya Chief Kidulile pamoja na watendaji wengine wakielekea kukagua madarasa na wanzi.
Baadhi ya wananchi wakitawanyika  baada ya kumaliza mkutano na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga

 Wanafunzi wa shule ya sekondari Chief Kidulile wakiwa wamekusanyika kwa pamoja kumsikiliza mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (hayupo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...